| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Jakaya Kikwete atahadharisha kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Sudan Kusini
Rais huyo mstaafu wa Tanzania, ameuomba Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa kusaidia kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa amani ili kuepuka kuvuruga makubaliano ya amani ya mwaka 2018 na kuzuia taifa hilo kurejea kwenye mizozo.
Jakaya Kikwete atahadharisha kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Sudan Kusini
Rais Mstaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete. / Others

Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Afrika (AU) nchini Sudan Kusini, Jakaya Kikwete, ameuomba Umoja wa Mataifa (UN) kusaidia kuhakikisha uchaguzi unaotarajiwa kufanyika nchini humo mwezi ujao unafanyika kwa amani bila vitendo vya vurugu.

Kikwete, ambaye pia ni Rais mstaafu wa Tanzania, ametoa ombi hilo kupitia mkutano wa video mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Jumanne, akieleza kuwa licha ya makubaliano ya amani ya mwaka 2018 yaliyomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka mitano, nchi hiyo bado inakabiliwa na mapigano ya silaha, vurugu na kuhama kwa wananchi kutoka makazi yao.

Amesisitiza umuhimu wa kufanyika kwa mageuzi katika sekta ya usalama na kuendelezwa kwa mazungumzo baina ya pande zote baada ya uchaguzi, ili kusaidia kurejesha umoja na kuponya majeraha ya taifa hilo, akionya kuwa, endapo uchaguzi huo hautaendeshwa kwa usahihi na kwa amani, Sudan Kusini inaweza kukumbwa na mgogoro mkubwa zaidi wa kisiasa na kiusalama, hali inayoweza kuhatarisha zaidi makubaliano ya amani yaliyopo.

CHANZO:TRT Afrika Swahili