| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Klabu ya 1860 Munich ya nchini Ujerumani yaelekea kufilisika
1860 Munich, ambao ni waasisi wa ligi ya Bundesliga, wamewahi kushinda taji la ligi hiyo mwaka 1966.
Klabu ya 1860 Munich ya nchini Ujerumani yaelekea kufilisika
1860 Munich, ambao ni waasisi wa ligi ya Bundesliga, wamewahi kushinda taji la ligi hiyo mwaka 1966./Picha:Reuters

Mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu ya Ujerumani, maarufu kama ‘Bundesliga’, klabu ya 1860 Munich imeanza mchakato kujitangaza kufilisika.

Katika taarifa yake ya Alhamisi, klabu hiyo, ambayo kwa sasa inashiriki ligi daraja la nne, ilisema kuwa, tayari imemteua mtu ambaye atahusika na kusimamia mchakato huo.

1860 Munich, ambao ni waasisi wa ligi ya Bundesliga, wamewahi kushinda taji la ligi hiyo mwaka 1966.

Hata hivyo, timu hiyo ilianza kupoteza mwelekeo katika ligi kuu ya Bundesliga katikati ya miaka ya 2000, ikikumbwa na ukata wa kifedha, kabla ya kushuka hadi daraja la tatu na hatimaye daraja la nne.

CHANZO:AFP