| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Erdogan apongeza mazungumzo ya amani ya Urusi na Ukraine jijini Istanbul kama 'hatua muhimu'
Matamshi ya rais wa Uturuki yanafuatia hatua nyingine ya mazungumzo ya Urusi na Ukraine jijini Istanbul, ambayo aliyapongeza licha ya mashambulizi ya Ukraine ya hivi karibuni ya ndege zisizokuwa na rubani dhidi ya miundombinu ya kijeshi ya Urusi.
Erdogan apongeza mazungumzo ya amani ya Urusi na Ukraine jijini Istanbul kama 'hatua muhimu'
"Ningependa pia kumleta [Rais wa Marekani Donald] Trump,” Erdogan alisisitiza. / AA

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amejitolea kuwa mwenyeji wa mkutano utakaojumuisha viongozi wa Urusi, Ukraine, pamoja na Marekani, kufanya jiji la Istanbul kuwa "kituo cha amani."

Akizungumza baada ya mkutano wa baraza la mawaziri siku ya Jumatatu, Erdogan amesema “matarajio yake makubwa" ni kuwaleta pamoja Rais wa Urusi Vladimir Putin na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy jijini Istanbul au Ankara.

"Ningependa pia kumleta [Rais wa Marekani Donald] Trump,” alisisitiza, huku wajumbe wa Urusi na Ukraine wakikutana jijini Istanbul kwa hatua ya pili ya majadiliano.

Erdogan alitangaza kuwa mkutano wa viongozi kuja pamoja nchini Uturuki, pia “atakutana nao kwenye mkutano huo ili kufanya jiji la Istanbul kuwa kituo cha amani.”

Alipongeza mazungumzo ya Jumatatu kama “hatua muhimu” licha ya matukio ya Jumapili nchini Urusi, yaliyohusisha mashambulizi ya angani usiku ya Ukraine kwa kutumia ndege 162 zisizokuwa na rubani, zikilenga zaidi ya ndege za kijeshi za Urusi 40, ikiwemo A-50, Tu-95, na Tu-22M3 zenye uwezo wa kubeba silaha za nyuklia.​​​​​​​

Yanayoendelea nchini Syria

Akizungumzia kuhusu Syria, alisema: “Huku Syria ikiendelea kupata ustawi na amani, tunaamini kuwa majirani zake na nchi zote kwenye kanda hii watafaidika kutokana na hili”.

Erdogan aliridhishwa na uamuzi wa mataifa ya Ulaya kuwaondolewa vikwazo Syria.

Rais wa Uturuki alitangaza,kuwa pamoja na kampuni ya Uturuki ya AJet kufanya safari zake za mara kwa mara za ndege kuelekea Syria, shirika la ndege la Syria Airlines pia litaanza safari zake za ndege hadi Uturuki hivi karibuni.

CHANZO:AA
Soma zaidi
Katika picha: Uturuki yaadhimisha miaka 103 ya Jamhuri
Uturuki yaadhimisha miaka 103 ya Siku ya Jamhuri kwa sherehe za kitaifa
“Uturuki ina nguvu zaidi leo kuliko jana,” asema Rais Erdogan katika maadhimisho ya Siku ya Jamhuri
Uturuki yasema ipo tayari kuingia mkataba wa majini na Misri
Erdogan ataka uongozi imara ndani ya Umoja wa Mataifa
Bunge la Uturuki lauidhinisha mkataba wa Makkah
Erdogan aapa kutetea haki za bahari za Uturuki, atoa wito wa umoja wa Libya
Biashara, ushirikiano wa anga kuwa sehemu ya ajenda ya mkutano wa nchi za Kiturki
Katika Siku ya UN, Erdogan wa Uturuki ataka Baraza la Usalama liwe 'la haki na shirikishi'
Ukiukaji wa Israel huko Gaza unadhoofisha imani katika mfumo wa kimataifa: Fidan
Uturuki yaandaa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa R4 kuhusu usalama wa kikanda
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki akutana na wenzake wa Uingereza na Pakistan
Erdogan aahidi kuendeleza diplomasia katika Kongamano la 9 la Upatanishi la Istanbul
Uturuki na Canada zalenga kuinua kiwango cha biashara hadi Dola bilioni 10
Rais Erdogan aipongeza Libya kwa kuidhinisha makubaliano ya mipaka ya bahari na Uturuki
Uturuki kudumisha uwepo wake wa kijeshi Syria na Iraq hadi usalama wa mipaka utakapoimarishwa
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Fidan na mkuu wa NATO Rutte wajadili usalama wa Bahari Nyeusi
Erdogan: Uturuki imefanikiwa kutibua njama za kuitumbukiza katika vita vya kikanda
Uturuki, Saudi Arabia zajadiliana usalama wa kikanda
Fidan wa Uturuki ataka umoja wa Kiislamu na ushirikiano zaidi na Iraq katika biashara na usalama