Magaidi wawaua watu 15, ikiwemo wanajeshi, kaskazini mashariki mwa Nigeria
Magaidi wamewaua wanajeshi wasiopungua 12 na raia watatu katika mashambulizi ya usiku kaskazini mashariki mwa Nigeria, vyanzo vya kijeshi na wakazi vilisema siku ya Jumatatu.
Magaidi wamewaua wanajeshi wasiopungua 12 na raia watatu katika mashambulizi ya usiku kaskazini mashariki mwa Nigeria, vyanzo vya kijeshi na wakazi vilisema siku ya Jumatatu.
Mashambulizi hayo maeneo ya Kukawa, Dalwa na Goniri yamekuja siku kadhaa baada ya shambulio kama hilo katika kituo cha jeshi huko Ngoshe.
Magaidi wa Boko Haram walishambulia wilaya ya Kukawa katika jimbo la Borno kabla ya alfajiri siku ya Jumatatu, na kupamabana na wanajeshi wa kambi ya karibu kwa saa tatu, wanajeshi waliokuwepo wameiambia Reuters.
Baadaye wanajeshi wakafanikiwa kudhibiti tena kambi lakini kamanda wao na wanajeshi wengine watano waliuawa, chanzo cha kijeshi kilisema. Karta Maina Ma'aji Lawan, mjumbe anaewakilisha Kukawa, alithibitisha mashambulizi hayo na kifo cha afisa huyo.
Nigeria yazidisha mashambulio dhidi ya magaidi
Huko Dalwa, magaidi waliwaua wanajeshi wawili na wakazi watatu kabla ya kuchoma moto nyumba zaidi ya 250, Shetima Isa, mkazi na kiongozi wa kijadi, alisema.
Katika jimbo jirani la Yobe, magaidi walishambulia kambi ya kijeshi ya Goniri, na kuwaua wanajeshi wanne na kuchoma magari na majengo moto, mwanajeshi mmoja alisema.
Jeshi la Nigeria limezidisha mashambulio katika maficho ya magaidi mwaka huu ikiwa ni sehemu ya mapambano mengine.
Mashambulizi ya sasa hivi yamekuja saa chache baada ya taarifa za kijasusi za jeshi kuonya kuhusu shambulio la kigaidi.