| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Erdogan: Uturuki itatumia jitahada zote kulinda mipaka na anga zake
Kauli ya Rais Erdogan inakuja mara baada ya NATO kutungua kombora la Iran lililokuwa linaelekea katika anga ya Uturuki.
Erdogan: Uturuki itatumia jitahada zote kulinda mipaka na anga zake
Rais Erdogan wa Uturuki./Picha:AA
4 Machi 2026

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema kuwa Uturuki inafanya kila liwezekanalo kulinda mipaka na anga zake, huku mgogoro katika kanda ukiendelea.

“Hatutoacha kitu linapokuja suala la usalama wa mipaka na anga katika nyakati hizi,” alisema Erdogan siku ya Jumatano.

Kiongozi huyo wa Uturuki alisema kuwa nchi yake inafanya kazi kwa ukaribu na NATO na washirika wake, na ilipo tayari kuchukua hatua kwa tishio lolote.

“Uturuki inachukua hatua zote za muhimu kwa kushirikiana na NATO kuchukua hatua pale inapohitajika,” alisema.

Kauli ya Rais Erdogan inakuja mara baada ya NATO kutungua kombora la Iran lililokuwa linaelekea katika anga ya Uturuki, kulingana na Wizara ya Ulinzi ya Uturuki.

Muda mfupi baadaye, Uturuki ikamwita balozi wa Iran nchini humo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan akifanya mazungumzo ya simu na  mwenzake wa Iran, Abbas Araghchi.

Onyo kali

Akizungumzia tukio hilo, Erdogan alisema Uturuki ilitoa onyo kali kwa Iran, kuachana na kitendo kama hicho katika siku zijazo.

“Tumeazimia kuhakikisha usalama wan chi yetu kwa kiwango chochote kile,” alisema.

Kulingana na Erdogan, uimarishwaji wa amani wa Uturuki, unahitaji uimarishwaji wa uwezo wa kiusalama.

“Kama taifa tunataka kuishi katika amani na utulivu, ni lazima tuimarishe hilo,” alisema Erdogan.

CHANZO:AA
Soma zaidi
Uturuki yaadhimisha miaka 106 ya shirika la habari la Anadolu
Rais wa Uturuki atoa salamu za Pasaka kwa jamii ya Wakristo
Erdogan, mkuu wa NATO wajadili mizozo kama 'mkwamo wa kijiografia' unaozidi kuongezeka juu ya Iran
'Wapinzani wa kudumu': Kwa nini nafasi ya Uturuki inayokua ya NATO inaifanya Israel kuwa na wasiwasi
Uturuki yaadhimisha miaka 77 ya NATO, yathibitisha jukumu la kimkakati katika muungano
Erdogan amuambia Putin ya kwamba Uturuki inapinga mashambulio dhidi ya Iran
Uturuki yaonya vita vya Mashariki ya Kati vinaweza kuenea katika eneo hilo, yatoa wito wa diplomasia
Israel ndiyo inayowajibika kwa kiasi kikubwa katika vita visivyo halali dhidi ya Iran: Rais Erdogan
Uturuki yalaani sheria ya hukumu ya kifo ya Israel dhidi ya Wapalestina na kuitaja kuwa ya batili
Kalin wa Uturuku awapokea wajumbe wa Hamas kujadili mpango wa amani wa Gaza
Ikiongozwa na Mke wa Rais wa Uturuki Emine Erdogan, dunia inaadhimisha Siku ya taka sufuri
Stratcom 2026 inakamilika mjini Istanbul kwa wito wa mawasiliano yanayotegemea ukweli
Vita vya Israel na Marekani dhidi ya Iran vinahatarisha mzozo wa kikanda: Mkuu wa ujasusi wa Uturuki
Fidan wa Uturuki: Vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran ni “kinyume cha sheria”
Vita visivyo na maana Mashariki ya Kati vinaathiri binadamu wote: Erdogan
Mkutano wa Stratcom 2026 wafunguliwa Istanbul wakati mvutano wa kimataifa ukiongezeka
Rais Erdogan atadhaharisha mfumo wa baada ya Vita ya Pili ya Dunia kupoteza uhalali wake
Uturuki haitokaa kimya wakati Israel inalitumbikiza eneo zima katika umwagaji damu: Erdogan
Hakan Fidan wa Uturuki aongoza juhudi za kusitisha vita vya Mashiriki ya Kati
Rais wa Uturuki na mwenzake wa Kazakhstan wajadili uhusiano wa mataifa mawili, masuala ya kikanda