| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Mwanaharakati na mjumbe wa amani Malala Yousafzai aitembelea Tanzania
Mshindi huyo wa tuzo ya amani ya Nobel, yupo Tanzania akihimiza elimu kwa watoto wa kike.
Mwanaharakati na mjumbe wa amani Malala Yousafzai aitembelea Tanzania
Mwanaharakati wa masuala ya elimu kwa watoto wa kike, Malala Yousafzai./Picha:Getty

Mwanaharakati wa mambo ya elimu na mjumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa, Malala Yousafzai yupo nchini Tanzania kwa shughuli maalumu ya kuhimiza elimu kwa watoto wa kike nchini humo.

Malala, ambaye alipokea tuzo ya amani ya Nobel, Oktoba 10, 2014, ameanza aliwasili nchini Tanzania, Julai 9, 2025 kama sehemu ya kampeni yake ya kuhakikisha watoto wa kike wanapata fursa ya elimu.

"Ni mara yangu ya kwanza kufika Tanzania. Nitakuwa nasherehekea siku ya Malala nikiwa katikati ya jamii za Watanzania, nikiwaunga mkono watoto wa kike wa Tanzania, nikipaza sauti zao na pia nikijifunza kutokana na mafanikio yao,” alisema Malala katika taarifa yake rasmi.

Kulingana na taarifa ilichapishwa kwenye tovuti ya taasisi ya Malala, katika ziara yake, mwanaharakati huyo anakutana na viongozi wa serikali, wadau wa elimu, hususani wale wanaohusika na elimu kwa mtoto wa kike na kujionea namna sanaa na michezo inavyotumuka kukuza elimu na uelewa ndani ya jamii za Tanzania.

 Mwaka 2013, Umoja wa Mataifa uliidhinisha Julai 12 kama ‘Siku ya Malala’, ili kutambua jitihada zake za kuhakikisha wanafunzi wa kike wanapata fursa za elimu.

Azimio hili lilipitishwa baada ya mwanaharakati huyo kuponea jaribio la kuuwawa na kikundi Taliban wakati akirudi nyumbani kutokea shuleni, akiwa na umri wa 15 tu.

Soma zaidi
Niger yawasilisha ombi la kujiondoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC
Polisi wa Wanyamapori nchini Kenya wamewakamata washukiwa 3 wa ujangili wakiwa na meno 6 ya tembo
Ufaransa yarekodi maambukizi ya kwanza ya Ebola kwa daktari aliyerejea kutoka DR Congo
Majengo ya jadi ya jamii ya Asante nchini Ghana
Libya yapiga marufuku kuingia kwa raia wa mataifa manne ya Afrika
Kenya yatia saini mkataba wa dola bilioni 1.2 na kampuni ya China kwa upanuzi wa uwanja wa ndege
Tanzania: Young Africans yaitolea macho mechi dhidi ya Azam FC
Familia ya Lungu kuamua atakapozikwa: Mahakama yaamuru
Waziri wa afya wa Kenya aagiza kusimamishwa mara moja kwa ujenzi wa Kituo cha Ebola cha Wamarekani
Vyuo vikuu 10 bora Afrika: Afrika Kusini inaongoza katika viwango vya hivi karibuni
Goli la kipindi cha pili lawapa Algeria ushindi dhidi ya Jordan Kombe la Dunia
Waziri wa Afya wa Kenya 'alidharau mahakama' kwa kuruhusu ujenzi wa kituo cha Ebola cha Marekani
Sudan Kusini kufanya Uchaguzi Mkuu Disemba 22
Sudan inatazamia Uturuki kuongeza umakini wa kimataifa huku vita vikiingia mwaka wa nne
Mbunge wa zamani wa Ghana ajeruhiwa kwa risasi nyumbani kwao
Afrika Kusini imewafukuza raia wa Malawi 5,000 katika kukabiliana na uhamiaji
2 wafariki kutokana na moto wa Soko la Gikomba Nairobi huku timu za uokoaji zikishutumiwa
Salah ahamasisha Misri kuifunga New Zealand 3-1 katika ushindi wa kihistoria Kombe la Dunia
UN yaonya juu ya 'hatari ya kutokea ukatili mkubwa' katika mji wa El-Obeid nchini Sudan
Moto wateketeza soko la Gikomba Nairobi huku waokoaji wakikimbizana kuokoa mali