Greenland isitumike katika njama ya kurubuni wengine

Kwa Trump kutumia ushuru kurubuni washirika kunadhihirisha uhusiano tete kati ya Marekani na Ulaya, na kuonesha tofauti zilizopo.

By
Mmoja ya waandamanji akiwa nje ya ubalozi mdogo wa Marekani huko Nuuk / AP

Na Sona Muzikarova

Jukwaa la Dunia la Kiuchumi la mwaka huu huko Davos ni la tofauti hasa kwa uhusiano wa Marekani na Ulaya. Rais Donald Trump anaonekana kama mchochezi wa masuala ya siasa na uchumi kati yao na Ulaya kuhusu suala la Greenland ambalo linatishia kuleta mgawanyiko.

Kile kilichoanza kama Marekani kuanzisha tena chokochoko ya kudhibiti Greenland – hatua ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikipingwa na Denmark – na sasa inaonekana kutumia ushuru kurubuni mataifa ya Ulaya: Asilimia 10 kuanzia mapema mwezi Februari, na kuongezea hadi asilimia 25 kufikia katikati ya mwaka, labda majadiliano kuhusu mustakabali ya kisiwa hicho yakubali matakwa ya Marekani.

Ulaya imejibu kwa umoja, ikionya kuhusu “kuzorota kwa hali,” na kuwa na kauli moja miongoni mwa nchi wanachama wa EU na NATO, ikiwemo Denmark, Ujerumani, Ufaransa, Uingereza, Norway, Finland, Uholanzi, na Sweden. Zaidi ya hayo, kuzungumzia mtazamo wa Marekani lazima utakabiliwa na pingamizi, EU inatafakari kuhusu kulipiza ushuru kwa bidhaa za Marekani wa hadi dola bilioni 109.

Hata nyumbani Marekani, msimamo wa Donald Trump kuchukua udhibiti wa Greenland umeshtumia na vyama vyote viwili, huku baadhi ya wabunge wa bunge la Congress wa chama cha Republican wakionya dhidi ya kufuatilia suala hilo, ambalo huenda ikamaanisha mwisho wa NATO.

Davos haitotatua mzozo huu, lakini itatoa nafasi ya wachokozi kuona hatari na matokeo ya hatua yao.

Kwa Marekani, kurubuni washirika kuhusu kufikia makubaliano kwa kutumia ushuru inakiuka misingi ya miungano ambayo kihistoria yamedhihirisha uwezo wa Marekani. Kwa Ulaya, kufahamu umuhimu wao wa kimkakati siyo suala la kujifurahisha lakini la msingi zaidi kiuchumi na kiusalama.

Mkakati wa Trump wa ushuru kwa Greenland unaweza ukasabisha kumalizika kwa ushirikiano kati ya Marekani na Ulaya.

Historia inaonesha kuwa nchi zenye uwezo mkubwa duniani hazifanikiwa kwa kuwarubuni marafiki zao na kwamba miungano inayumba kwa muda mrefu kabla ya kusambaratika. Kwa msingi huu Davos, siyo sehemu ya kujadili kwa malengo ya kurubuni, lakini kwa kutambua mustakabali wa mataifa ya Magharibi unategemea zaidi utashi wa nidhamu ya pamoja kuliko hotuba za utamaduni wa pamoja.