Mashambulizi ya Marekani-Israeli yalenga bwawa la maji kusini-magharibi mwa Iran
Maafisa wa Iran wanasema mashambulio yamegonga kituo muhimu cha maji huku mivutano ya kieneo ikiendelea kuongezeka.
Mashambulizi yanayoendelea ya Marekani na Israel yamelenga hifadhi ya maji huko Haftkel katika mkoa wa Khuzestan kusini magharibi mwa Iran, vyombo vya habari vya Iran vimeripoti.
Bwawa hilo la maji lenye ukubwa wa mita za ujazo 10,000 limelengwa katika mashambulkio yaliyofanyika Jumamosi jioni, shirika la serikali la Iran IRNA lilisema, likimnukuu Valiollah Hayati, naibu gavana.
Uhasama katika eneo hilo umeongezeka tangu Marekani na Israel zianzishe vita vya pamoja dhidi ya Iran mnamo Februari 28, hadi sasa na kuua zaidi ya watu 1,340, akiwemo Kiongozi Mkuu wa wakati huo Ali Khamenei.
Tehran imejibu mawimbi ya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani na makombora yakilenga Israel, Jordan, Iraq na nchi za Ghuba zinazohifadhi mali za kijeshi za Marekani, na kusababisha hasara na uharibifu wa miundombinu huku ikivuruga masoko ya kimataifa na usafiri wa anga.
Waswasi wa kikanda
Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Ujasusi la Uturuki, MIT, ameonya kwamba vita vinavyoendelea vinavyohusisha Israel, Marekani, na Iran vinaweza kuzidi kuwa mzozo mkubwa wa kimataifa iwapo vitaendelea.
Akizungumza katika Mkutano wa STRATCOM 2026 huko Istanbul Jumamosi, Ibrahim Kalin alisema: "Tangu janga hili, ulimwengu wetu umekuwa ukipitia vizingiti vingi muhimu, mizozo na milipuko."
Kalin pia alisema matokeo ya vita vya mauaji ya halaiki ya Israel dhidi ya Gaza vilivyoanza Oktoba 7, 2023 yanaendelea kushuhudiwa.
"Wakati juhudi za kuleta amani huko Gaza zikiendelea, ukiukwaji wa Israel na sera zake za kuikalia kwa mabavu na unyakuzi unaendelea bila kukatizwa," alisema.