Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inatarajiwa kuwapokea wahamiaji zaidi ya 30 kutoka Marekani wiki hii, vyanzo vinne viliiambia Reuters siku ya Jumanne.
Wahamiaji hao siyo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Wengine wanatoka Marekani ya Kati na Kusini, kulingana na chanzo kimoja na nyaraka za mahakama ya Marekani.
Chanzo kimoja kinachofahamu yanayojiri kinasema idadi ya wahamiaji hao itakuwa 37, huku kingine kikisema idadi hiyo itakuwa 45.
Watakuwa wahamiaji wa kwanza kufika kwenye nchi hiyo ya Afrika ya Kati ikiwa ni sehemu ya makubaliano na serikali ya Trump yaliyotangazwa Aprili 5.
Madini
Hatua hii inasadifu na juhudi za Marekani kutekeleza mpango wa amani walioratibu kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda yenye wenye lengo la kumaliza mapigano mashariki mwa DRC.
Makubaliano ya kuwasafirisha wahamiaji pia yanafuata kutia saini ushirikiano wa kimkakati unaowapa uhuru Marekani wa kuchimba madini muhimu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
DRC inasema haitolipia gharama yoyote
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewahi kusisitiza kuwa haitotumia fedha zake kama sehemu ya makubaliano ya nchi ya tatu inayokubali wahamiaji kutoka Marekani.
Marekani imewahi kuwapeleka wahamiaji katika mataifa ya Afrika ikiwemo Ghana, Cameroon, Equatorial Guinea, na Eswatini.











