Pakistan yashambulia mji mkuu wa Afghanistan, na mikoa mengine

Uongozi wa Pakistan umeapa "kuchukua hatua kali" kwa tishio lolote dhidi ya mipaka ya nchi huku mapigano na nchi jirani ya Afghanistan yakiongezeka.

By
Vyanzo vya usalama nchini Pakistani vilisema ghala la silaha na kituo cha usafirishaji viliharibiwa wakati wa mashambulizi huko Kandahar. / Reuters

Jeshi la Pakistan limefanya mashambulizi ya anga katika sehemu kadhaa za Afghanistan, ikiwa ni pamoja na mji mkuu wa Kabul, na majimbo ya Kandahar na Paktia, kulingana na msemaji wa serikali ya Afghanistan.

Taarifa ya Afghanistan ilisema vikosi vya Pakistan vilifanya mashambulizi ya angani yaliyolenga “baadhi ya maeneo,” huku milipuko mingi mikubwa ikiripotiwa katikati ya jiji la Kabul mapema siku ya 27 Februari.

Huku msemaji wa serikali ya Afghanistan akidai hakuna majeruhi walioripotiwa kutokana na mashambulizi hayo, msemaji wa Waziri Mkuu wa Pakistan, alisema mashambulizi yao yamewaua wanajeshi 133 wa Afghanistan na kuwajeruhi zaidi ya 200.

Aliongeza kuwa vikosi vya Pakistani vimeharibu vituo 27 vya kijeshi vya Afghanistan, makao makuu mawili ya vikosi, na zaidi ya vifaru na magari ya kivita 80.

Vyanzo vya usalama nchini Pakistani vilisema ghala la silaha na kituo cha usafirishaji viliharibiwa wakati wa mashambulizi huko Kandahar.

Wakati huo huo, Wizara ya Ulinzi ya Afghanistan ilisema oparesheni za kulipiza kisasi za vikosi vya Afghanistan zinazolenga maeneo ya Pakistani katika mpaka wa Durand zilimalizika usiku wa manane.

Mapema Alhamisi, takriban wanajeshi wanane wa Afghanistan na wawili wa Pakistani waliuawa wakati wa mashambulizi ya mpakani yaliyodumu kwa saa nne.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameelezea wasiwasi wake kuhusu mapigano hayo.