| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Trump: Putin hataishambulia nchi yoyote iliyoko ndani ya NATO
Trump pia amekanusha taarifa za vyombo vya habari kwamba Mkurugenzi wa CIA, John Ratcliffe, aliionya Urusi kuhusu uwezekano wa kuishambulia ardhi ya NATO.
Trump: Putin hataishambulia nchi yoyote iliyoko ndani ya NATO
Rais Trump akizungumza katika na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House mnamo Agosti 27, 2026. /

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kuwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin, hataishambulia nchi yoyote mwanachama wa NATO.

Trump pia amekanusha taarifa za vyombo vya habari kwamba Mkurugenzi wa CIA, John Ratcliffe, aliionya Urusi kuhusu uwezekano wa kuishambulia ardhi ya NATO.

Trump amesema hayo siku ya Alhamisi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi ya Oval ya Ikulu ya Marekani.

“Hataishambulia ardhi ya NATO,” Trump aliwaambia waandishi wa habari.

Mapema siku hiyo, Trump aliliambia shirika la habari la Axios katika mahojiano kwa njia ya simu kwamba hakutakuwa na shambulio kama hilo. Pia alikanusha taarifa kwamba Ratcliffe alikuwa ametumwa kwenda Urusi kwa lengo la kufikisha ujumbe maalumu kwa viongozi wa Urusi.

“Ratcliffe hukutana na mwenzake wa Urusi mara moja kila baada ya miezi sita au mara moja kwa mwaka. Wana uhusiano mzuri sana. Hakukuwa na ujumbe wowote, na hakukuwa na jambo lolote lisilo la kawaida,” Trump aliiambia Axios

CHANZO:Reuters