| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Rais Samia wa Tanzania atoa onyo dhidi ya uharibifu wa mali za umma
Rais Samia amesema serikali inatumia fedha nyingi kujenga miundombinu.
Rais Samia wa Tanzania atoa onyo dhidi ya uharibifu wa mali za umma
Rais Samia amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika kulinda mali za umma. /ikulu_Tanzania / X

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametoa onyo kali dhidi ya uharibifu wa mali za umma, hususan miundombinu, akisisitiza kuwa serikali hutumia miaka mingi kutafuta fedha za kujenga na kuendeleza miradi hiyo.

Akizungumza, Rais Samia amesema: "Hatuwezi kutumia miaka mingi kutafuta fedha za kujenga miundombinu na kuanza kutoa huduma, halafu tukakubali juhudi hizo ziharibiwe ndani ya muda mfupi. Hili halikubaliki."

Aidha, amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika kulinda mali za umma.

"Ninawaomba wananchi, ninyi wenyewe muwe walinzi wa mali hizi. Mtu anayeharibu mali za umma anateketeza kodi za wananchi. Anayefanya hivyo anachelewesha maendeleo ya taifa, analirudisha nyuma taifa, ni mhujumu wa taifa letu na ni adui wa taifa letu," amesema.

Rais Samia alitoa kauli hiyo leo katika hafla ya uzinduzi wa miundombinu ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) Awamu ya Pili, iliyofanyika eneo la Temeke, Azizi Ali, mkoani Dar es Salaam.

CHANZO:TRT Afrika
Soma zaidi
Aliyekuwa afisa wa ujasusi Uganda arejeshwa Marekani kukabiliwa na mashtaka ya magendo
Mlipuko wa ugonjwa wa kimeta waua viboko 46 na tembo wanane nchini Zambia
Mwenge wa Olimpiki wawasili Senegal kwa ajili ya Olimpiki barani Afrika
Putin anaunga mkono juhudi za Afrika za kutaka mageuzi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Niger yamteua mkuu mpya wa jeshi baada ya jaribio la uasi lililozimwa
Mfalme Oyo Nyimba kuzikwa leo kwa mujibu wa mila na desturi
Putin na Ramaphosa wajadili uhusiano kati ya Urusi na Afrika Kusini katika mkutano wa BRICS
Rais wa Zimbabwe Mnangagwa atangaza siku yake ya kuzaliwa kuwa sikukuu ya kitaifa
Bunge la Nigeria lasitisha safari za wajumbe wake Afrika Kusini kufuatia vurugu dhidi ya wahamiaji
Uchaguzi wa Nigeria 2027: Tinubu vs Atiku
Algeria yaizuia UAE kutumia anga yake baada ya kusitisha uhusiano wa kidiplomasia
Mahakama yakataa ombi la Lissu kumuita Rais Samia kutoa ushahidi
Algeria yasitisha uhusiano wake wa kidiplomasia na UAE
Ufalme wa Uganda wamteua mtangazaji wa televisheni kumrithi Mfalme Oyo Nyimba
Mufti Mkuu Tanzania atoa wito kwa Waislamu kufunga siku tatu kuomba kuepushwa na madhara ya El Nino
Umoja wa Mataifa wapongeza makubaliano ya Libya kuelekea katika uchaguzi
Putin amuambia Trump: Urusi haina nia ya kuzishambulia nchi za Ulaya
Wahamiaji zaidi ya 1,000 waokolewa pwani ya Afrika magharibi ndani ya wiki moja, MSF inasema
Ghana yasema imetumia $4.37 milioni kuwarudisha raia wake nyumbani kutoka Afrika Kusini
Waburundi waomba nyaraka za kusafiria kufuatia operesheni dhidi ya wafanyabiashara wa kigeni Kenya