Makosa ya golikipa wa Senegal Khady Faye kumpa nafasi ya goli Melissa Bethi lililowapa Algeria ushindi wa 2-0 siku ya Jumapili katika mechi za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON).
Bethi alifunga katika dakika ya 88 kuongeza katika goli lilofungwa na nahodha Marine Dafeur kupitia mkwaju wa penati katika dakika ya 42.
Algeria ilianza mechi hiyo wakipewa nafasi kubwa kutokana na kuorodheshwa bora kuliko Senegal barani Afrika na wakiwa nafasi tano mbele zaidi katika orodha ya dunia.
Utata wa penati
Penati waliopewa Algeria na mwamuzi wa Afrika Kusini ilikuwa na utata kutokana na kuwa nahodha wa Senegal Korka Fall na Amira Braham hawakuwa wamegusana.
Baada ya tathmini ya VAR, kiungo wa Bristol City Dafeur alifunga penati hiyo.
Morocco yaigaragaza Kenya
Wenyeji Morocco waliwafunga Kenya 4-0 katika mechi yao ya kwanza ya kundi A uwanja wa Moulay El Hassan jijini Rabat siku ya Jumapili.
Ibtissam Jraidi alifunga magoli mawili, huku Sakina Ouzraoui na Meriem Atiq wakifunga goli moja kila mmoja wakati Atlas Lionesses wakipata matokeo ya kuridhisha mbele ya mashabiki wa nyumbani.
Matokeo hayo yaliiweka timu hiyo ya kocha Jorge Vilda kuongoza kundi A ikiwa na tofauti ya magoli na Algeria.
Mabingwa mara 10 Nigeria inacheza mechi yake ya kwanza ya kundi C dhidi ya Malawi siku ya Jumanne, ambayo ni madada mawili wachezaji nyota. Tabitha Chawinga anacheza klabu ya Lyon na Temwa Chawinga yuko katika timu ya Kansas City Connect.
Mashindano hayo yaliyoanza Jumapili Julai 26 Julai yatamalizika Agosti 16.















