Kocha wa Morocco Mohamed Ouahbi ameahidi kuwa timu yake itaimarika zaidi baada ya kutolewa kwenye hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia na Ufaransa siku ya Alhamisi.
Simba hao wa Atlas walitarajia angalau kufika nusu fainali kama ilivyokuwa nchini Qatar 2022, lakini kwa mara nyingine tena Les Bleus ndiyo waliokwamisha ndoto zao za Kombe la Dunia.
Ushindi wa magoli 2-0 katika uwanja wa Gillette katibu na mji wa Boston ilikuwa marudio ya matokeo wakati timu hizo zilipokabiliana katika nusu fainali miaka minne iliopita, na sasa Morocco inaangazia majukumu yake mengine baada ya miezi saba iliopita iliokuwa na heka heka nyingi.
"Ufaransa ni timu nzuri sana. Tulikuwa tunacheza na nchi ambayo imefuzu kwa fainali mbili zilizopita za Kombe la Dunia, na wameimarika zaidi sasa hivi," alikiri Ouahbi, baada ya timu yake kufungishwa virago kwa magoli mawili ya kipindi cha pili kutoka kwa Kylian Mbappe na Ousmane Dembele.












