| swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Safari ya siasa ya Raila Odinga
Safari ya Raila Odinga katika siasa ilianza miongo kadhaa iliyopita.
Safari ya siasa ya Raila Odinga
Aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga. / Reuters
15 Oktoba 2025

Katika miaka ya sabini alifanya kazi na Shirika la Viwango Kenya na kuwa Naibu Mkurugenzi.

Mwaka 1982 alikamatwa na kushtakiwa kwa uhaini baada ya kuhusishwa na jaribio la mapinduzi lililoongozwa na wanajeshi ambao walinasibishwa naye.

Alifungwa jela na kuachiwa huru baada ya miaka sita lakini akakamatwa tena muda mfupi baadaye na kuachiwa miezi michache baadaye mwaka 1989.

Akakamatwa tena mwaka 1990 akiwa pamoja na wanaharakati wa wanasiasa waliokuwa wanapigania kuondolewa kwa mfumo wa utawala wa chama kimoja.

Aliachiliwa 1991 na akakikimbia nchi na kuelekea Norway akidai kuwa serikali ilikuwa inapanga njama ya kumuua.

Miaka kadhaa baadaye katika kitabu alichoandika kuhusu maisha yake ya siasa alikiri kuhusika katika jaribio hilo la mapinduzi kwa kiasi kikubwa.

Baadhi ya wanasiasa walitaka ashtakiwe tena kwa uhaini ila kisheria muda wa mashtaka kuanzishwa tena ulikuwa umepita.

Miongoni mwa waliofungwa pamoja naye wakati wa harakati zake za kutaka demokrasia ni wanasiasa  Kenneth Matiba na aliyekuwa meya wa jiji la Nairobi Charles Rubia.


Raila Odinga alirejea nchini Kenya mwaka 1992 wakati huo akijiunga na chama alichokianzishwa baba yake Jaramogi Oginga Odinga, FORD  na ndiyo mwaka ambapo uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi ulifanyika nchini Kenya.

Raila alishinda ubunge wa jimbo la Langata, lakini baba yake hakufanikiwa kushinda urais dhidi ya Daniel arap Moi.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Soma zaidi
Kiongozi wa zamani wa waasi wa DRC anayeshtakiwa Paris kwa uhalifu wa kivita aanza mgomo wa kula
UN yaagiza uchunguzi wa dharura ufanyike kuhusu ukiukaji wa sheria katika Al Fasher ya Sudan
Rais wa Tanzania atangaza uchunguzi kuhusu mauaji ya waandamanaji katika uchaguzi
Wakimbizi 57,000 wamewasili kaskazini mwa Sudan baada ya mashambulizi ya RSF huko Darfur, Kordofan
Afrika Kusini yaruhusu kuingia kwa wakimbizi zaidi ya 150 kutoka Gaza, Palestina
Afrika yakumbwa na mlipuko wa kipindupindu mbaya zaidi katika miaka 25
Mataifa ya G7 walaani mashambulizi ya RSF dhidi ya raia Sudan, watoa wito wa kusitishwa mapigano
Wakenya zaidi ya 200 wajiunga na jeshi la Urusi
AU yakanusha tuhuma za Trump kuhusu mauaji ya halaiki Nigeria
Mwigulu Nchemba ateuliwa Waziri Mkuu Tanzania
Jaji Mkenya achaguliwa Mahakama ya Kimataifa ya Haki
Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amfuta kazi makamu wake
Duma wa Botswana aipa India zawadi ya duma 8
Kesi ya Roger Lumbala wa DRC yaanza kusikilizwa
Kesi za ubakaji, watoto kupotea zaripotiwa Darfur, Sudan – Umoja wa Mataifa
Ugonjwa wa Kichaa cha mbwa barani Afrika: Janga linaloendelea kuathiri maisha japo linaepukika
Libya yatakiwa kufunga vituo vya kuwazuilia wahamiaji katika mkutano wa Umoja wa Mataifa
Rais Museveni aonya kuzuka kwa vita endapo nchi za Afrika zitashindwa kufikia Bahari ya Hindi
UN: Milioni 11 wanawake na wasichana wanabeba uzito mkubwa wakati njaa ya Sudan inaendelea kupamba moto
Ethiopia yachagguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa, COP32