| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz azomewa baada ya kuzinadi sera za serikali
Moja wa washiriki wa kongamano hilo, alimjia juu kiongozi huyo kufuatia matamshi yake ya hivi karibuni ya kuwataka Wajerumani waongezewe muda wa kufanya kazi.
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz azomewa baada ya kuzinadi sera za serikali
Kansela Friedrich Merz wa Ujerumani./Picha:Reuters / Reuters

Kansela Friedrich Merz wa Ujerumani alijikuta kwenye wakati mgumu siku ya Ijumaa, baada ya kuzinadi sera za serikali ya Ujerumani.

Kansela huyo alizomewa wakati wa kongamano la Wakatoliki katika eneo la Wurzburg, baada ya baadhi ya washiriki kuonesha kutopendezwa na sera za kiuchumi na mazingira za serikali ya Ujerumani.

Moja wa washiriki wa kongamano hilo, alimjia juu kiongozi huyo kufuatia matamshi yake ya hivi karibuni ya kuwataka Wajerumani waongezewe muda wa kufanya kazi.

Mshiriki huyo, pia aliikosoa serikali ya Ujerumani ya kubadilisha mfumo mzima wa mifuko ya hifadhi ya jamii, akilalamikia kupanda kwa gharama za maisha chini humo.

“Hakuna mtu yeyote ndani ya chama change aliyewahi kusema kuwa Wajerumani ni watu wavivu,” alisema Merz.

CHANZO:AA