| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amtimua Waziri wa Fedha baada ya siku kadhaa ofisini
Waziri wa Fedha alikuwa ameshika wadhifa huo kwa chini ya wiki mbili, huku kipindi cha Mkuu wa Keshi kilikubwa na kuongezeka kwa hali ya ukosefu wa usalama.
Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amtimua Waziri wa Fedha baada ya siku kadhaa ofisini
Sudan Kusini imekuwa ikikumbwa na changamoto katika kutekeleza kikamilifu mageuzi muhimu yaliyoainishwa katika makubaliano ya amani ya mwaka 2018./ / AP

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, amemfuta kazi Mkuu wa Jeshi la nchi hiyo pamoja na Waziri wa Fedha ambaye alikuwa ametumikia nafasi hiyo chini ya wiki mbili, vyombo vya habari vya serikali nchini humo viliripoti usiku wa Jumatano.

Hatua hizo ni sehemu ya mabadiliko ya mara kwa mara katika safu za juu za serikali ya Salva Kiir katika miaka ya hivi karibuni.

Mkuu wa Jeshi aliyefutwa kazi, Jenerali Paul Nang, alikuwa ameshika nafasi hiyo tangu Oktoba 2025, na uongozi wake ulikuwa ukikosolewa zaidi kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama nchini. Kwa upande wake, Waziri wa Fedha, Salvatore Garang Mabiordit, alikuwa ametumikia nafasi hiyo tangu Aprili 23 mwaka huu.

Deng Wol ateuliwa kwa mara ya pili

Salva Kiir amemteua tena Jenerali Santino Deng Wol kuwa mkuu mpya wa jeshi, shirika la habari la serikali la South Sudan Broadcasting Corporation lilisema. Wol, ambaye anatoka eneo la Bahr El Gazal ambako Kiir pia anatokea, ni mshirika wa karibu wa rais na aliwahi kushika nafasi hiyo kati ya mwaka 2020 na 2024.

Kuol Daniel Ayulo, mtaalamu wa muda mrefu serikalini ambaye aliwahi kufanya kazi katika wizara ya fedha na wizara ya biashara kama katibu mkuu msaidizi, ameteuliwa kuwa waziri mpya wa fedha, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali.

Sudan Kusini imekuwa ikikumbwa na changamoto katika kutekeleza kikamilifu mageuzi muhimu yaliyoainishwa katika makubaliano ya amani ya mwaka 2018 yaliyomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka mitano, ikiwa ni pamoja na kuunganisha majeshi ya nchi na kuandaa uchaguzi.

CHANZO:AFP
Soma zaidi
Uturuki na Algeria wasisitiza ushirikiano wa kimkakati wakati wa mkutano wa Erdogan-Tebboune
Rais wa DRC asema yuko tayari kugombea muhula wa tatu 'kama wananchi watataka'
Umoja wa Mataifa waonya kuhusu hali tete eneo linalozozaniwa kati ya Sudan na Sudan Kusini
Rigathi Gachagua arudi mahakamani kusikiliza kesi ya kupinga kuondolewa madarakani
Uturuki yalaumu mashambulizi ya Boko Haram yaliyowaua wanajeshi 23 Chad
Afrika Kusini yasema 'haina ubaguzi'
Uturuki, Kenya yatia saini makubaliano ya ushirikiano wa  ulinzi katika maonesho ya Istanbul expo
Nigeria, Marekani wazindua vikosi kazi vya ulinzi kukabiliana ukosefu wa usalama
Tanzania: Gharama za mafuta zazidi kupanda
Afrika Kusini inatambua aina ya hantavirus inayohusishwa na meli ya kitalii
Rais wa Algeria Tebboune kuwasili Uturuki kwa ziara rasmi ya siku tatu
Burkina Faso yapiga marufuku NGO zaidi, kufikisha idadi ya mashirika 205
Burkina Faso yapiga marufuku kituo cha televisheni cha Ufaransa kwa 'upotoshaji'
Shambulio la kigaidi la Boko Haram katika kambi ya jeshi Chad laua watu wasiopungua 24
Ghana kuwa mwenyeji wa kongamano la dunia kuhusu fidia kwa watumwa
Shirika la Afya Duniani (WHO) lathibitisha maambukizi ya kirusi cha Hanta
Rais wa Taiwan asema hawatokubali kukandamizwa baada ya ziara yake ya Eswatini
Zambia yasema matamshi ya balozi wa Marekani anayeondoka 'si ya kidiplomasia'
Jeshi la Sudan linasema limeangusha droni zilizokuwa zimeelekezwa uwanja wa ndege wa Khartoum
Kiongozi wa Mali Assimi Goita achukua majukumu ya waziri wa ulinzi baada ya kifo cha aliyekuwepo