Mahakama Kuu ya Nepal imetoa kibali cha kulima bangi kwa ajii ya matumizi ya kitabibu, kitafiti na kisayansi.
Hata hivyo, Mahakama hiyo imeitaka serikali ya Nepal kuandaa kanuni maalumu zitakazodhibiti kilimo na uzalishaji wa zao hilo ambalo limepigwa marufuku katika baadhi ya mataifa duniani.
"Tunaishukuru Mahakama Kuu kwa uamuzi huu,” alisema Saroj Adhikari, mmoja ya waleta pingamizi la kutaka kuruhusu uzalishwaji wa zao hilo.
Nepal ilisitisha utoaji leseni kwa wauzaji wa bangi nchini humo mwaka 1973, kufuatia shinikizo la Marekani.
Hata hivyo, kabla ya hapo, Nepal ilijizolea umaarufu wa kuwa eneo lililoshamiri kwa biashara ya bangi kutoka kwa wauzaji waliopewa vibali na serikali ya nchi hiyo.
Uamuzi huo, umepokelewa vizuri na waziri wa zamani wa afya wa Nepal, Birodh Khatiwada, ambaye kwa muda mrefu, alipigania kuondolewa kwa zuio hilo.
"Baada ya muda mrefu wa kusubiri, hatimaye uamuzi umetoka,” alisema Khatiwada.
"Nchi nyingi zilizoendelea zimepitisha kilimo cha bangi, hakuna sababu yeyote ya sisi kuchelewesha hilo,” aliongeza.
Nchini Nepal, historia ya kilimo cha bangi inaanzia mbali, ikianzia wakati zai likitumika katika vyakula na tiba asilia.
Kila mwaka, mamia ya watu hukutana mbele ya hekalu la Pashupatinath, kwa ibada ya mungu Shiva, huku wakivuta bangi.



















