| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Dangote aanza kuuza mafuta kwa Dola za Marekani nchini Nigeria kutokana na uhaba wa mafuta ghafi
Kiwanda cha Dangote cha kusafisha mafuta nchini Nigeria kimeanza kuuza mafuta katika soko la ndani kwa Dola za Marekani.
Dangote aanza kuuza mafuta kwa Dola za Marekani nchini Nigeria kutokana na uhaba wa mafuta ghafi
Kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote ndicho kikubwa zaidi barani Afrika, kikiwa na uwezo wa kusafisha mapipa 700,000 kwa siku. / / Reuters

Kiwanda cha Dangote cha kusafisha mafuta nchini Nigeria kimeanza kuuza mafuta kwa Dola za Marekani katika soko la ndani, ikieleza kuwa imefikia uamuzi huo kutokana na ugumu wa kupata mafuta ghafi ya kutosha kupitia mpango wa serikali wa kununua mafuta ghafi kutumia sarafu ya Naira, pamoja na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la kimataifa.

Akizungumza siku ya Jumanne, msemaji wa kampuni alisema kuwa upungufu wa mafuta ghafi yanayotolewa chini ya mpango huo umeifanya kampuni ishindwe kuendelea kuuza mafuta kwa sarafu ya Nigeria, Naira, wakati inanunua malighafi kwa Dola za Marekani.

Mpango wa kununua mafuta ghafi kutumia sarafu ya Naira, ulioanzishwa Oktoba 2024, ulilenga kuwaruhusu wasafishaji wa mafuta nchini kununua mafuta ghafi kwa kutumia sarafu ya Nigeria, naira, ili kupunguza matumizi ya fedha za kigeni na kuimarisha soko la ubadilishaji wa fedha.

Kiwanda cha Dangote, ambacho ni kikubwa zaidi barani Afrika na kina uwezo wa kusafisha mapipa 700,000 ya mafuta ghafi kwa siku, kimeweka bei mpya za bidhaa zake ambapo petroli itauzwa kwa Dola 0.779 kwa lita, dizeli kwa dola 1.087 kwa lita, na mafuta ya ndege kwa Dola 0.942 kwa lita. Bei hizo zimo kwenye jedwali la bei lililotolewa kwa wasambazaji wa mafuta.

Makamu wa Rais wa Dangote Group, Edwin Devakumar, alisema kampuni imekuwa ikibeba mzigo wa tofauti ya thamani ya sarafu kwa kuuza mafuta kwa Naira huku ikinunua mafuta ghafi kwa Dola za Marekani. Hata hivyo, alisema upatikanaji mdogo wa mafuta ghafi kupitia mpango wa kununua mafuta ghafi kutumia Naira umeufanya mfumo huo ushindwe kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi.

Mahitaji ya Dola yanatarajiwa kuongezeka

Ingawa Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Nigeria (NNPC) iliongeza kiwango cha mafuta ghafi kinachopelekwa Dangote hadi shehena saba mwezi Mei kutoka wastani wa shehena tano hapo awali, kampuni hiyo imesema inahitaji kati ya shehena 13 na 15 kila mwezi ili kuendesha shughuli zake kikamilifu.

Uamuzi huo unaweza kuongeza mahitaji ya dola miongoni mwa wauzaji wa mafuta na kufanya bei za mafuta za ndani kuwa nyeti zaidi kwa mabadiliko ya viwango vya ubadilishaji wa fedha.

Kutokana na upungufu huo, imelazimika kuagiza mafuta ghafi yaliyobaki kutoka soko la kimataifa kwa bei za kimataifa.

CHANZO:Reuters
Soma zaidi
Rais wa Afrika Kusini aagiza hatua za kuwalinda wanawake kufuatia mfululizo wa mauaji
Misri yakana kuingilia mambo ya ndani ya Ethiopia na kuunga mkono makundi yenye silaha
Edward Kijanangoma atawazwa mfalme mpya wa Tooro
Je, Afrika itapata viti vya kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa?
Jeshi la Polisi Tanzania laonya wanaochochea mgomo wa madereva wa mabasi
Madaktari bingwa wa Tanzania waweka kambi ya matibabu Malawi
Makamu wa Rais Tanzania ataka vijana kupewa fursa za mafunzo ya ajira
Jeshi la Sudan lapinga madai ya kuunga mkono makundi ya upinzani Ethiopia
Uchaguzi Mkuu kurejesha utulivu Sudan Kusini?
Marekani italazimika kuondoka Mashariki ya Kati: Iran
Mashambulizi ya kigaidi mjini Mogadishu yapungua kwa karibu asilimia 90: Serikali ya Somalia
Maambukizi ya Ebola nchini DRC ni zaidi ya 8,000 tangu kuanza kwa mlipuko huo
Watoto 17 miongoni mwa wahamiaji 250 waliookolewa katika pwani ya Mauritania
Marekani kusitisha ufadhili wa sekta ya afya nchini Zimbabwe kufikia mwishoni mwa mwezi wa Septemba
Mwanamke wa kumi apatikana amefariki katika msururu  wa mauaji nchini Afrika Kusini
Qatar Airways yakopesha marubani kwa shirika la ndege la taifa la Rwanda
Wapiganaji wa RSF wahamia upande wa jeshi la Sudan baada ya kushuhudia 'maafa'
Mkuu wa Umoja wa Mataifa asikitishwa kwa kunyimwa viza  kiongozi wa Sudan, Burhan kuhudhuria UNGA
Jenerali wa DR Congo miongoni mwa watu 13 waliofariki katika ajali ya ndege
Afrika itapata hadhi ya uwanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama Umoja wa Mataifa?