Rais Erdogan atuma salamu za Ramadhan kwa taifa na ulimwengu wa Kiislamu

Rais Recep Tayyip Erdogan ameonesha matumaini kwamba mwezi mtukufu utadumisha umoja na kuleta baraka kwa binadamu.

By
Rais Erdogan alipohudhuria mkutano wa magavana iliyofanyika Ikulu Ankarakk. / AA / TRT Afrika Swahili

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan Jumatano alituma salamu zake za mwezi mtukufu wa Ramadhan, akielezea matumaini yake kuleta baraka na umoja wa taifa, ulimwengu wa Kiislamu, na kwa binadamu kwa ujumla.

Alituma salamu zake kupitia mtandao wa kijamii wa Kituruki NSosyal, na kusema kuwa mwezi mtukufu “unaleta mambo mazuri kwa nchi yetu, ulimwengu wa Kiislamu na binadamu wote.”

Rais amekielezea kipindi hicho kama "siku zenye baraka ambapo milango ya rehema hufunguliwa” na kuomba idumishe umoja.

Erdogan pia ameomba “siku hizi zenye baraka zidumishe umoja wetu.”