tokea masaa 2
Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif ameelekea Saudi Arabia, siku moja baada ya kuwa na mazungumzo ya simu na rais wa Iran.
Katika ziara hiyo, Sharif atafanya mazungumzo na mwana mfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman.
Kati ya mambo mengine, wawili hao watajadiliana mzozo unaoendelea katika kanda hiyo pamoja na hali ya usalama kwa ujumla.
ZILIZOPENDEKEZWA
Ziara hiyo inakuja siku moja baada ya Sharif kufanya mazungumzo ya simu na Rais Masoud Pezeshkian wa Iran, ambaye alimueleza waziri mkuu wa Pakistan, kuwa njia pekee ya kumaliza mashambulizi ya Marekani-Israel dhidi ya Iran ni kupitia kutambua haki za msingi za Iran.
Septemba mwaka jana, Pakistan na Saudi Arabia zilitiliana saini mkataba wa ulinzi.
CHANZO:AA
















