UTURUKI
2 dk kusoma
Mke wa Rais wa Uturuki aadhimisha miaka miwili ya mauaji ya halaiki Gaza, atoa wito wa umoja
Erdogan anasema kuwa katika kipindi cha miwili, Gaza imekuwa sehemu ya makaburi ambapo watu zaidi ya 67,000 wasio na hatia, ikiwemo watoto zaidi 20,000, wameuawa.
Mke wa Rais wa Uturuki aadhimisha miaka miwili ya mauaji ya halaiki Gaza, atoa wito wa umoja
Erdogan anasema kuwa miaka miwili iliopita, Gaza imekuwa sehemu ya makaburi. / AA
7 Oktoba 2025

Mke wa Rais wa Uturuki Emine Erdogan ameadhimisha miaka miwili ya mauaji ya halaiki ya Israel huko Gaza, akishtumu Israel kwa kujaribu kuangamiza watu wa Palestina huku dunia ikiangalia.

“Taifa ambalo limepoteza dira yake ya maadili linataka kuangamiza watu wa Palestina huku dunia ikiangalia,” amesema Erdogan katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Uturuki NSosyal.

“Na huku unyama wa wanaodhulumu ukiongezeka, na ndivyo sauti za mioyo ya watu iliyoungana zinavyopazwa dhidi ya mauaji ya halaiki,” aliongeza.

Erdogan amesema kuwa katika kipindi cha miaka miwili, Gaza imekuwa sehemu ya makaburi ambapo watu zaidi ya 67,000 wasio na hatia, ikiwemo watoto zaidi ya 20,000, wameuawa, na utu wa ubinadamu umezikwa ukiwa hai.

Alisisitiza kuwa mashambulizi ya Israel, “hakuna mipaka yoyote si ya heshima, sheria, haki za binadamu, au maadili ambayo haijakiukwa.”

Amesema watu wamejitolea kusaidia Gaza kutoka kila pembe ya dunia, kwa ndege, njia za ardhini, na kwa bahari, pengine akiashiria kuhusu msafara wa meli za misaada za hivi karibuni katika bahari ya mediterani kuelekea eneo hilo ambalo limezingirwa, na kutoa wito “kwa kila mtu aliyeguswa na hili kuungana kwenye harakati hizi kwa pamoja kwa ajili ya Palestina hadi pale amani ya haki na ya kudumu itakapopatikana.”

“Naadhimisha kuwatakia rehma ndugu zetu wa Palestina waliokufa mashahidi kutokana na mashambulizi ya Israel, na naomba Allah Mtukufu kuwafanyia wepesi na kuwapa ushindi watu wa Palestina majasiri ambao, kwa subira yao, wanaendelea kuwa imara. #EndlessGenocideGaza,” alisema.

Ujumbe huo pia ulijumuisha video zilizoonesha hotuba za zamani za Erdogan kuhusu Gaza pamoja na video zilizoonesha namna gani hali ilivyo mbaya katika kanda hiyo.

CHANZO:AA
Soma zaidi
Ujumbe wa Erdogan 'Azerbaijan haiko peke yake' ulipelekea ushindi wa Karabakh: Aliyev
Ushindi wa Karabakh wa Azerbaijan kwa amani ya Caucasus: Rais Erdogan
Uturuki yatoa hati ya kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Netanyahu, juu ya mashtaka ya mauaji
Erdogan: Uturuki kuharakisha miradi ya kiulinzi kuimarisha ‘maslahi’ na washirika wa Ulaya
Uturuki kuandaa mazungumzo ya Gaza wiki ijayo kufuatia wasiwasi juu ya usitishaji mapigano – Fidan
Mfumo wa ulimwengu wa sasa unazingatia nguvu zaidi ya haki: Mkurugenzi wa TRT
Israel imeigeuza Gaza kuwa vifusi, inawezaji kuwa haina hatia: Erdogan
Uturuki yakashifu unafiki wa nchi za Magharibi kuhusu Gaza, yatoa wito wa mfumo mpya wa dunia
Hamas haina nuyklia, Israel iko nayo: Erdogan aitaka Berlin ichukue hatua kali dhidi ya Tel Aviv
Erdogan ataka kuona mabadiliko katika uhusiano na EU na ushirikiano wa kikanda alipokutana na Mertz
Ujerumani yatoa wito wa kuunda “ushirikiano wa kimkakati” ili kukabiliana na changamoto za kimataifa
"Marekebisho ya Ulimwengu": Jukwaa la 9 la TRT World kuanza Istanbul likiangazia majadiliano na haki
Erdogan ametangaza washindi wa Tuzo Kuu za Utamaduni na Sanaa za Urais mwaka 2025
Uturuki yaadhimisha miaka 102 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri
Uturuki yatoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano katika mji wa Al Fasher, Sudan
Uturuki na Jordan zasaini makubaliano ya kuimarisha uhusiano wa kiuchumi
Erdogan atangaza kukabidhiwa kwa jeshi vifaru vya kwanza  vya Altay vilivyotengenezwa Uturuki
Israel inaishutumu 'Uturuki chini ya utawala wa Erdogan’ kuwa na uhasama mkali dhidi yake
Erdogan na Starmer wasaini mkataba wa ndege za kivita za Eurofighter Typhoon
Erdogan, amkaribisha Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, katika Ikulu ya Ankara