| swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Azimio la Gaza latoa wito wa uvumilivu, heshima na ustawi wa pamoja
Erdogan, Trump, Sisi, na Sheikh Tamim wamesaini nchini Misri azimio la kumaliza vita vya Gaza, wakati wa Mkutano wa Amani wa Sharm el-Sheikh.
Azimio la Gaza latoa wito wa uvumilivu, heshima na ustawi wa pamoja
Viongozi wa dunia, wakiwemo Trump, Erdogan, Macron na Mfalme Abdullah, wakipiga picha kwenye mkutano wa Sharm el-Sheikh wa kusitisha mapigano Gaza. /
13 Oktoba 2025

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan, Rais wa Marekani Donald Trump, Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi, na Emir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani wamesaini nchini Misri tamko la nia ya kumaliza vita vya Gaza, wakati wa Mkutano wa Amani wa Sharm el-Sheikh. Viongozi hao wamekubaliana kwamba amani ya Gaza lazima ijengwe juu ya misingi ya usawa na kuheshimiana.

“Tunasisitiza uvumilivu, heshima na fursa sawa kwa wote,” walisema viongozi hao katika azimio hilo lililosainiwa Jumatatu mjini Sharm el-Sheikh, Misri.

“Tunataka eneo hili liwe mahali ambapo kila mtu anaweza kufuatilia ndoto zake kwa amani, usalama na ustawi wa kiuchumi, bila kujali rangi, dini au kabila.”

Azimiio hilo liliongeza kuwa viongozi hao “wanalenga mtazamo wa kina wa amani, usalama na ustawi wa pamoja” unaojikita katika kuheshimiana na hisia ya umoja.

“Kwa roho hiyo, tunakaribisha maendeleo yaliyopatikana katika kuanzisha makubaliano ya amani ya kudumu na ya kina Gaza, pamoja na uhusiano wa kirafiki na wenye manufaa kwa pande zote kati ya Israel na majirani zake wa kikanda,” viongozi walisema katika azimio hilo.

Viongozi hao wameonyesha kuwa tayari na kufanya kwa pamoja bega kwa bega ili kutekeleza na kudumisha mafanikio haya, kwa kuweka misingi ya taasisi itakayowawezesha vizazi vijavyo “kustawi pamoja kwa amani.”

“Tuko tayari kwa mustakabali wa amani ya kudumu,” walisema.

Awamu ya kwanza ya makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza ilianza kutekelezwa Ijumaa, chini ya mpango wa Trump wa kukomesha vita vya miaka miwili vya Israel dhidi ya eneo hilo.

Mapema Jumatatu, wafungwa wa Kipalestina waliokuwa magerezani Israel walianza kuachiwa, baada ya Hamas kuachilia Waisraeli 20 waliokuwa bado hai waliokuwa wametekwa Gaza.

Tangu Oktoba 2023, mashambulizi ya kinyama ya Israel yamewaua zaidi ya Wapalestina 67,800 huko Gaza — wengi wao wakiwa wanawake na watoto — na kufanya eneo hilo lisiwe na makazi ya binadamu kuweza kuishi kutokana na uharibifu mkubwa.

CHANZO:TRT World
Soma zaidi
Uturuki inamkumbuka Ataturk miaka 87 baada ya kufariki
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki kuzuru Marekani siku ya Jumatatu
Rais Erdogan anatumai Marekani itatimiza ahadi zake kuhusu makubaliano ya ndege za kivita za F-35
Palestina inapongeza amri za kukamatwa dhidi ya maafisa 37 wa Israel kutoka Uturuki kama 'ushindi
Ujumbe wa Erdogan 'Azerbaijan haiko peke yake' ulipelekea ushindi wa Karabakh: Aliyev
Ushindi wa Karabakh wa Azerbaijan kwa amani ya Caucasus: Rais Erdogan
Uturuki yatoa hati ya kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Netanyahu, juu ya mashtaka ya mauaji
Erdogan: Uturuki kuharakisha miradi ya kiulinzi kuimarisha ‘maslahi’ na washirika wa Ulaya
Uturuki kuandaa mazungumzo ya Gaza wiki ijayo kufuatia wasiwasi juu ya usitishaji mapigano – Fidan
Mfumo wa ulimwengu wa sasa unazingatia nguvu zaidi ya haki: Mkurugenzi wa TRT
Israel imeigeuza Gaza kuwa vifusi, inawezaji kuwa haina hatia: Erdogan
Uturuki yakashifu unafiki wa nchi za Magharibi kuhusu Gaza, yatoa wito wa mfumo mpya wa dunia
Hamas haina nuyklia, Israel iko nayo: Erdogan aitaka Berlin ichukue hatua kali dhidi ya Tel Aviv
Erdogan ataka kuona mabadiliko katika uhusiano na EU na ushirikiano wa kikanda alipokutana na Mertz
Ujerumani yatoa wito wa kuunda “ushirikiano wa kimkakati” ili kukabiliana na changamoto za kimataifa
"Marekebisho ya Ulimwengu": Jukwaa la 9 la TRT World kuanza Istanbul likiangazia majadiliano na haki
Erdogan ametangaza washindi wa Tuzo Kuu za Utamaduni na Sanaa za Urais mwaka 2025
Uturuki yaadhimisha miaka 102 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri
Uturuki yatoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano katika mji wa Al Fasher, Sudan
Uturuki na Jordan zasaini makubaliano ya kuimarisha uhusiano wa kiuchumi