Monaco waliongoza kipindi cha kwanza wakati Maghnes Akliouche alipoipatia goli timu hiyo ya ugenini.
Mechi ilibadilika kabla ya saa moja ya mechi wakati Mamadou Coulibaly alipooneshwa kadi nyekundu kwa kumchezea ‘‘rafu’’ Achraf Hakimi akiwa tayari ameoneshwa kadi ya njano dakika tatu kabla ya hapo.
PSG walisawazisha kupitia goli za Marquinhos.
Winga Kvaratskhelia aliongezea PSG bao la mbili katika dakika ya 66 kwa shuti la karibu baada ya kipa wa Monaco Philipp Kohn kuokoa mpira uliokuwa umepigwa na Hakimi.
Dakika za mwisho mwisho, Jordan Teze aliisawazishia Monaco kufanya matokeo kuwa 2-2 lakini ikawa ni ya kufutia machozi tu kwa ‘‘Le Rocher’’. Jumla ya matokeo kwa mechi zote mbili yalikuwa 5-4 kwa PSG.
Mabingwa hao sasa watakabiliana na Chelsea au Barcelona katika hatua inayofuata, na watafahamu kuhusu mpinzani huo katika droo itakayofanyika siku ya Ijumaa.









