| Swahili
ULIMWENGU
2 dk kusoma
Marekani yasitisha mashambulizi dhidi ya Iran kwa muda huku juhudi za kidiplomasia zikiendelea
Juhudi za kidiplomasia zinaendelea ili kupunguza mvutano katika mzozo kati ya Marekani na Iran, kwa mujibu wa afisa mmoja aliyelizungumza na CNN.
Marekani yasitisha mashambulizi dhidi ya Iran kwa muda huku juhudi za kidiplomasia zikiendelea
Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza ya kuwa makubaliano ya kusitisha vita yameisha. / / AFP

Juhudi za kidiplomasia zinaendelea nyuma ya pazia kwa lengo la kupunguza mvutano kati ya mataifa hayo mawili, kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa Ijumaa na CNN ikinukuu maafisa wa Marekani.

Afisa mmoja wa Marekani alisema kuwa mkakati wa Marekani umekuwa kufanya mashambulizi kwa wakati fulani kisha kuyasitisha kwa muda ili kuepusha ongezeko la mvutano na kutoa nafasi kwa juhudi za kidiplomasia kuendelea. Pia alisema Marekani inaendelea kuwa na orodha ya malengo inayotumika kama njia ya kuongeza ushawishi katika mazungumzo.

Kwa mujibu wa maafisa kadhaa, maandalizi ya uwezekano wa mashambulizi mapya ya Marekani yalikuwa yamefanyika kwa Ijumaa usiku endapo yangehitajika. Hata hivyo, kwa sasa kipaumbele kinatolewa kwa juhudi za kidiplomasia.

Mapema leo, ndani ya meli ya kivita ya USS Abraham Lincoln iliyoko katika Bahari ya Arabia, wahudumu wa anga waliandaa ndege za kivita kwa kuzipakia silaha huku marubani wakiendelea na mazoezi ya kujiandaa kwa operesheni zozote za mashambulizi zitakazoweza kuhitajika.

Nahodha wa meli hiyo aliwaeleza maelfu ya wanamaji waliomo ndani kwamba mvutano katika eneo hilo unaongezeka, na akasisitiza umuhimu wa kuendelea kuwa tayari wakati wote, jambo alilosema ni utaratibu wa kawaida wa kijeshi.

Sambamba na maandalizi hayo, marubani wa ndege za kivita waliendelea na operesheni za kawaida za ulinzi, wakifanya safari za doria mchana na usiku.

Maafisa wa Marekani pia walikanusha madai ya Iran kwamba tayari kulikuwa na mashambulizi mengine ya Marekani, wakisema taarifa hizo si sahihi.

Hata hivyo, waliongeza kuwa hali inaweza kubadilika kwa haraka na mashambulizi yanaweza kuanza tena endapo yatabainika kuwa ni muhimu.

CHANZO:Anadolu Agency
Soma zaidi
Mahakama Syria yamhukumu kifo Rais wa zamani Bashar al Assad
Zelensky: Urusi inaanda makombora kutoka Korea Kaskazini ili itushambulie
Anayetuhumiwa kumuua Tupac Shakur afikishwa mahakamani
Marekani yathibitisha kuiunga mkono Yemen katika vita dhidi ya Wahouthi
Israel 'yakataa' mpango wa Trump wa vipengele 15 kwa ajili ya Gaza, asema Waziri Mkuu Netanyahu
Mamia wanaandamana nchini Afrika Kusini kupinga ghasia dhidi ya wahamiaji
Israel yafuta vibali vya kuingia nchini kwa wanaharakati wa Marekani wanaowaunga mkono Wapalestina
Mkuu wa Mossad anasemekana kuwafuta kazi maafisa waandamizi kwa kushindwa kuipindua serikali ya Iran
Iran yatishia kushambulia mitambo ya umeme ya nchi za Ghuba iwapo Marekani itashambulia mitambo yake
Nchi 20 za Kiislamu zajadili hatua za pamoja dhidi ya ukiukaji wa Israel katika Msikiti wa Al-Aqsa
Mawaziri wa bara Arabu, Waislamu wakutana Jordan kujadili kwa pamoja Jerusalem Mashariki inayokaliwa
Wahamiaji 70,000 waondoka Hispania huku idadi ya vifo ikiongezeka
Wanafunzi wa Korea Kusini matatani kwa ‘kuvunja’ na kuingia ndani ya kambi ya kijeshi ya Marekani
Wahamiaji wapatao 160 waokolewa baada ya meli yao kuwaka moto
Chama cha soka cha Palestina chaituhumu FIFA kwa kushindwa kuiadhibu Israel
Trump aitaka Iran ichague kati ya makubaliano na kujislamisha
Namna kijana mwenye umri wa miaka 12 mwenye usonji alivyotumia uokaji keki kukabiliana na chuki
Australia yathibitisha vifo vya ndege vinavyotokana na mafua H5
Iran: Hatuna mazungumzo yoyote na Marekani
Mashambulizi ya Israel yaua Wapalestina 12, wakiwemo watoto wawili, huko Gaza