China kuziondolea ushuru nchi za Afrika ifikapo mwezi Mei
Hata hivyo, msamaha huo hautoihusu Eswatini, ambayo ina uhusiano wa kidiplomasia na Taiwan.
China inalenga kuziondolea nchi za Afrika ushuru, ifikapo mwezi Mei mwaka huu, rais wa nchi hiyo Xi Jinping amesema.
Kufikia sasa, China imeyaondolea ushuru mataifa 33 ya Afrika, huku ikisisitiza kuwa inalenga kuondoa tozo hizo kwa nchi nyingi zaidi barani humo.
Hata hivyo, msamaha huo hautoihusu Eswatini, ambayo ina uhusiano wa kidiplomasia na Taiwan.
Hii ni kutokana kwamba, China inadai kuwa kisiwa hicho ni mali yake.
Mataifa mengi ya Afrika kwa sasa, yanaiangalia China kama mshirika muhimu baada ya Marekani kuamua kuziwekea nchi za Afrika viwango vikubwa vya ushuru, mwaka jana.
Kulingana na Rais Xi, mpango wa kuziondolea ushuru nchi za Afrika, utatoa fursa kubwa za maendeleo kwa nchi hizo.