| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Tanzania kupata ufadhili wa Dola bilioni 2.33 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa reli
Tanzania inalenga kujenga reli ya kisasa ya zaidi ya  kilomita 2,561, kuunganisha nchi ya Afrika Mashariki na nchi jirani zisizo na bandari.
Tanzania kupata ufadhili wa Dola bilioni 2.33 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa reli
Tanzania inalenga kujenga reli ya kisasa ya zaidi ya kilomita 2,561. / Reuters

Tanzania imefanikiwa kupata ufadhili wa Dola bilioni 2.33 kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa yani Standard Gauge.

Benki ya Standard Chartered inasema imefanikiwa kupanga mpango wa ufadhili wa Dola bilioni 2.33 kwa mradi wa Reli ya Standard Gauge nchini Tanzania.

Pesa hizo zitafadhili sehemu mbili za njia ya reli iliyopangwa ya kilomita 1,219 inayounganisha mji mkuu wa kibiashara na bandari ya Dar es Salaam na jiji la Mwanza kando ya ziwa.

Kampuni ya Yapi Merkezi ya Uturuki itahusika katika ujenzi huo.

Shirika la Ujenzi la Uhandisi wa Kiraia la China litafanya kazi hiyo pia katika sehemu tofauti kulingana na taarifa ya Benki hiyo.

Ufadhili ulipatikana kutoka kwa mashirika ya mikopo ya nje, benki za biashara na taasisi za fedha za maendeleo, iliongeza.

“Ujenzi na uboreshaji wa reli ya kisasa ya Standard Gauge utaunganisha bandari ya Dar es Salaam na njia kuu za ukuaji katika maeneo ya magharibi mwa Tanzania na nchi jirani, na kutoa usafiri wa uhakika kwa watu na mizigo,” ilisema Benki hiyo. 

"SGR itachochea maendeleo ya kiuchumi ya maeneo ya ndani ya Tanzania."

Tanzania inalenga kujenga reli ya kisasa ya zaidi ya  kilomita 2,561, kuunganisha nchi ya Afrika Mashar na nchi majirani zisizo na bandari za Rwanda, Burundi, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

CHANZO:reuters