Uturuki imekuwa ikimkumbuka Balozi wake wa Sudan Kusini, Metin Ergin, aliefariki dunia siku ya Jumatatu akiwa na umri wa miaka 59.
"Napenda kutoa salamu zangu za rambirambi kwa familia yake, wapendwa wake na jamii yetu, na tunaomba Mungu amrehemu Balozi Ergin, ambaye alitumikia nchi yetu kwa miaka 35 kwa dhati," Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan alisema katika taarifa siku ya Jumanne.
Wizara ya Mambo ya Nje pia ilitoa salamu zake za rambirambi kufuatia kifo cha mwanadiplomasia huyo.
"Tunaskitika kutangaza kifo cha Novemba 2 2026 cha mwenzetu Metin Ergin (1967, Istanbul), ambaye amekuwa akifanya kazi katika Wizara yetu tangu 1992 na amewakilisha Taifa letu kama Balozi Mostar, Bosnia na Herzegovina na Antwerp, Ubelgiji, na kama Balozi nchini Sudan Kusini," wizara ilisema katika taarifa.
"Atazikwa katika makaburi ya Zincirlikuyu jijini Istanbul baada ya swala ya Ijumaa tarehe 6 Novemba 2026. Mungu ailaze roho yake pahali pema, na tunatoa salamu zetu za rambirambi kwa familia yake," iliongeza.
UTURUKI
1 dk kusoma
Balozi wa Uturuki nchini Sudan Kusini Metin Ergin afariki dunia
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan ameongoza katika kumkumbuka mwanadiplomasia huyo aliefariki siku ya Jumatatu.

Soma zaidi





















