| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Papa Leo XIV amkumbuka mtangulizi wake Papa Francis mwaka mmoja baada ya kifo chake
Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani alifanya kumbukizi hiyo wakati akizungumza na wanahabari akiwa ndani ya ndege yake wakati akitokea Angola kuelekea Equatorial Guinea.
Papa Leo XIV amkumbuka mtangulizi wake Papa Francis mwaka mmoja baada ya kifo chake
Kiongozi wa Kanisa Katoliki dunia Papa Leo XIV akizungumza na wanahabari ndani ya ndege yake./Picha:Reuters

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV amemkumbuka mtangulizi wake, Papa Francis, mwaka mmoja baada ya kifo chake.

Katika kumbukizi hiyo siku ya Jumanne, Papa Leo XIV amekumbuka huduma ya mtangulizi wake katika kuhubiri kuhusu huruma ya Mungu pamoja na hulka yake ya kukaa pamoja na watu wahitaji.

“Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya maisha ya Francis kwa kanisa na dunia nzima,” alisema Papa Leo.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani alifanya kumbukizi hiyo wakati akizungumza na wanahabari akiwa ndani ya ndege yake wakati akitokea Angola kuelekea Equatorial Guinea.

Papa Francis alifariki dunia Jumatatu ya Pasaka mwaka jana, baada ya kuugua ugonjwa wa kiharusi.

Alikutwa na umauti akiwa Vatican baada ya kutoka hospitali baada ya kuugua nimonia, licha ya kuweza kutoa baraka za Pasaka ndani ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

CHANZO:AP
Soma zaidi
Goli la kipindi cha pili lawapa Algeria ushindi dhidi ya Jordan Kombe la Dunia
Waziri wa Afya wa Kenya 'alidharau mahakama' kwa kuruhusu ujenzi wa kituo cha Ebola cha Marekani
Sudan Kusini kufanya Uchaguzi Mkuu Disemba 22
Sudan inatazamia Uturuki kuongeza umakini wa kimataifa huku vita vikiingia mwaka wa nne
Mbunge wa zamani wa Ghana ajeruhiwa kwa risasi nyumbani kwao
Afrika Kusini imewafukuza raia wa Malawi 5,000 katika kukabiliana na uhamiaji
2 wafariki kutokana na moto wa Soko la Gikomba Nairobi huku timu za uokoaji zikishutumiwa
Salah ahamasisha Misri kuifunga New Zealand 3-1 katika ushindi wa kihistoria Kombe la Dunia
UN yaonya juu ya 'hatari ya kutokea ukatili mkubwa' katika mji wa El-Obeid nchini Sudan
Moto wateketeza soko la Gikomba Nairobi huku waokoaji wakikimbizana kuokoa mali
Ghana yasherehekea mwisho wa utumwa kwa wito wa fidia
Wahamiaji 15 wamefariki dunia baada ya boti kuzama karibu na ufuo wa Libya
Kenya yatoa onyo kali dhidi ya ghasia zozote kabla ya maandamano yaliyopangwa kufanyika Juni 25
Vijana wa Kenya hawastahili kulazimishwa kubeba mzigo wa madeni ambao hawakutafuta
Mjumbe wa UN amtaka kiongozi wa RSF Dagalo kusitisha mashambulizi dhidi ya El-Obeid, Sudan
Mlipuko wa Ebola: Madaktari 17 wafariki huku virusi vikienea 'kwa kasi'
Safari za ndege zimerejea katika uwanja mkuu wa ndege wa Niger baada ya shambulio la kigaidi
Rais Netumbo Nandi-Ndaitwah wa Namibia aanza ziara rasmi Tanzania
Ubalozi wa Marekani nchini Kenya watoa tahadhari kuhusu maandamano ya Juni 25
Mshambuliaji wa Côte d'Ivoire Wahi hatimaye apata viza ya Canada baada ya kunyimwa awali