Jeshi la Somalia, vikosi vya Uganda vyashambulia magaidia wa Al Shabab

Jeshi la Somalia, likisaidiwa na vikosi vya Uganda vya AUSSOM, lilifanya operesheheni inayojulikana kama "Operation Rolling Thunder" kusini mwa Somalia kulenga ngome za kundi la kigaidi la Al Shabab.

By
Katika miaka ya hivi karibuni, jeshi la Somalia, limezidisha mashambulizi dhidi ya kundi la kigaidi la Al Shabab. / AA

Jeshi la Somalia, likisaidiwa na vikosi Umoja wa Afrika (AUSSOM) na washirika wengine wa kigeni, limefanya mashambulio yanayojulikana kwa jina la “Operation Rolling Thunder” kusini mwa Somalia yaliyolenga ngome za kundi la kigaidi la Al Shabab, taarifa kutoka Wizara ya Ulinzi ilisena siku ya Jumapili.

Wizara inasema vikosi hivyo vinpanga kuvunja ngome za Al Shabab eneo la Lower Shabelle na kukata kabisa njia ya kundi hilo lenye ushirikiano na Al Qaeda wanayotumia kwa shughuli zao za kigaidi.

Inasema oparesheni hiyo inalenga kudhoofisha uwezo wa Al Shabab, kumaliza njama zozote za mashambulizi, na kuwalinda raia katika maeneo muhimu ya kilimo.

Wizara hiyo imeahidi kuwa ‘‘Operation Rolling Thunder’’ itaendeleda hado pale kundi hilo la kigaidi “litakuwa limemalizwa kabisa kuondolewa kama tishio kwa amani, maendeleo, na ujenzi wa taifa la Somalia.”

Muda wa AUSSOM umeongezwa

Al Shabab imekuwa ikiendeleza ugaidi dhidi ya serikali ya Somalia kwa zaidi ya miaka 16, mara nyingi ikilenga maafisa wa usalama, wa serikali na raia.

Tangu mwezi Julai, jeshi la Somalia, likisaidiwa na AUSSOM na washirika wengine wa kimataifa, limezidisha oparesheni dhidi ya kundi hilo.

Muda wa AUSSOM umeongezwa kwa mwaka mmoja zaidi na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi Disemba, huku Uingereza ikiidhinisha had Disemba 31, 2026.