Rais wa Marekani, Donald amesema amepata taarifa ya kuwa ni Iran ndio walioangusha helikopta ya Marekani katika Mlango-Bahari wa Hormuz.
"Nimejulishwa hivi punde na Jeshi letu kwamba jana usiku Wairani wamedungua moja ya helikopta zetu za kisasa aina ya Apache wakati ikifanya doria juu ya Mlango-Bahari wa Hormuz. Kulikuwa na marubani wawili ndani yake, na wote wako salama bila majeraha yoyote. Hata hivyo, Marekani inalazimika kujibu shambulio hili", Rais Trump amesema kupitia mtandao wake wa kijamii wa Truth Social.
ZILIZOPENDEKEZWA
Tukio hili limetokea saa chache tu baada ya Iran na Israel kushambuliana siku ya Jumatatu, na hivyo kuhatarisha mazungumzo ya kuimarisha usitishaji mapigano ulioyumba.
CHANZO:TRT Afrika

















