Indonesia: Tutaheshimu utawala wa Iran chini ya Mojtaba Khamenei
Uteuzi wa Mojtaba Khamenei, unakuja baada ya kifo cha aliyekuwa kiongozi mkuu wa Iran, Ali Khamenei aliyeuawa na mashambuli ya Marekani-Israel.
Indonesia imesema kuwa itaheshimu utawala mpya wa Iran, ulio chini ya Mojtaba Khamenei.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo, Yvonne Mewengkang alisema kuwa serikali ya Indonesia inafuatilia kwa ukaribu yanayoendelea ndani ya Iran, hususani uteuzi wa Mojtaba.
Uteuzi wa Mojtaba Khamenei, unakuja baada ya kifo cha aliyekuwa kiongozi mkuu wa Iran, Ali Khamenei aliyeuawa na mashambuli ya Marekani-Israel.
“Indonesia inaheshimu utawala wa Iran na mchakato wake wa kikatiba,” alisema Yvonne.
Mbali na Indonesia, nchi nyingine zilizoutambua utawala huo mpya ni pamoja na Urusi, Iraq, Oman, Azerbaijan na Belarus.
Mgogoro unazidi kuongezeka katika eneo la Mashariki ya Kati mara baada ya Marekani na Israel kufanya mashambulizi ya pamoja dhidi ya Iran, ambayo yameua watu wapatao 1,300.