Rais wa Marekani Donald Trump amemshukuru Mfalme Mohammed VI wa Morocco baada ya nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika kuipa jina la Trump moja ya barabara kuu mpya nchini humo.
“Asante Mohammed VI, Mfalme wa Morroco unayeheshimika-ni heshima kubwa," Trump aliandika katika mtandao wake wa kijamii Truth Social Jumapili, pamoja na video ya barabara kuu ya "Rais Donald J. Trump."
Rais Trump amesema anatarajia "kusafiri katika barabara hiyo siku moja, pengine karibuni."
Barabara hiyo kuu ina urefu wa kilomita 1,055 kutoka Tiznit mpaka Dakhla, mji uliopo katika eneo lenye mgogoro Magharibi mwa Sahara.
Hatua hiyo inaonesha uhusiano wa karibu kati ya Marekani na Morocco.
Morocco ina makubaliano ya urafiki ya muda mrefu na Marekani katika historia, kuanzia 1786.















