| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Uganda yakanusha madai ya Marekani ya kufadhili kliniki za Ebola nchini humo
Wizara ya afya ya Uganda inasema haina taarifa kuhusu pale vituo hivyo vya matibabu vilipo katika nchi yao.
Uganda yakanusha madai ya Marekani ya kufadhili kliniki za Ebola nchini humo
PICHA YA MAKTABA: Daktari nchini Uganda akijiandaa kumpa chanjo mtu aliyetangamana na mgonjwa wa Ebola. / Reuters

Wizara ya afya ya Uganda imekanusha madai ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kuwa Marekani inafadhili ujenzi wa kliniki 50 katika maeneo yaliyoathiriwa na Ebola nchini humo.

Mlipuko ulipatikana mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Ijumaa iliopita na unashukiwa kusababisha vifo vya watu 139 na maambukizi karibu 600.

Maambukizi mawili pia yamethibitishwa katika nchi jirani ya Uganda.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ametangaza Jumanne kuwa wameahidi kufadhili vituo 50 vya kutibu Ebola katika maeneo yaliyokumbwa na mlipuko huo nchini DRC na Uganda.

‘Hatuna taarifa hizo’

Lakini wizara ya afya ya Uganda ilisema siku ya Jumatano kuwa haijawahi kujadili kuhusu ujenzi wa vituo vya matibabu.

Katika taarifa, wizara ilisema "haina taarifa ya pale vituo hivyo vilipo nchini mwao".

“Tunaendelea kuthibitisha kuwa Uganda imebaini maambukizi mawili ya Ebola kutoka nje kufikia sasa: mtu mmoja amefariki na mwingine bado anatibiwa. Hakuna maambukizi ya ndani ya nchi na hali ni shwari kwa sasa,” taarifa ilisema.

Marekani imepiga marufuku raia wasiokuwa wa Marekani ambao wametoka DRC, Uganda au Sudan Kusini katika siku 21 zilizopita kuingia nchini kwao kutokana na mlipuko.

CHANZO:TRT Afrika
Soma zaidi
Ebola: Mkutano wa India na Afrika wa jijini New Delhi waahirishwa
Urusi yaeleza wasiwasi wake kuhusu mlipuko wa Ebola huku Korea Kusini ikitoa tahadhari kwa Uganda
DRC yaongeza uchunguzi wa Ebola katika mji wa Goma unaodhibitiwa na M23
DRC yasitisha mazoezi ya Kombe la Dunia kufuatia hofu ya Ebola
Kesi ya Félicien Kabuga yafutwa rasmi ndani ya Mahakama ya Umoja wa Mataifa
Sierra Leone yakubali kupokea kundi la kwanza la wahamiaji wanaofukuzwa Marekani
Viongozi kadhaa wa Afrika wameipongeza timu ya Arsenal kwa kushinda ubingwa wa EPL
Wanajeshi saba wa Nigeria wauawa katika shambulio la kigaidi
Bahrain yapiga marufuku wageni kutoka DRC, Uganda kwa kuhofia ugonjwa wa Ebola
Rais Samia ataka jamii ielimishwe kuhusu matumizi ya nishati ya nyuklia
Mgomo wa usafiri wa umma Kenya kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta wasitishwa
Mjumbe wa zamani wa Ubelgiji anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya Patrice Lumumba afariki
Mkenya aliyeacha uhandisi na kujikita kwenye tasnia ya sanaa
Mgomo wa usafiri wa umma nchini Kenya waingia siku yake ya pili, wanne wafariki
Jukwaa la Kidiplomasia la Antalya kwa mtazamo wa viongozi wa Afrika
Tanzania: Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya Ghasia Oktoba 29
Ugonjwa wa Ebola waahirisha maadhimisho ya Siku ya Mashahidi wa Uganda
Mwanamke aliyechomwa na moto kwa sababu ya kujichora sura ya Rais Ruto afariki dunia
Rais Mwinyi aishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kuipatia misaada ya maendeleo Zanzibar
WHO yaanza mkutano wake wa kila mwaka huku kukiwa na tatizo la Ebola DRC