| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Urusi yaeleza wasiwasi wake kuhusu mlipuko wa Ebola huku Korea Kusini ikitoa tahadhari kwa Uganda
Urusi inasema iko tayari kutatua tatizo hilo huku Korea Kusini ikiwaomba raia wake kufuta au kuahirisha safari zao za kwenda Uganda.
Urusi yaeleza wasiwasi wake kuhusu mlipuko wa Ebola huku Korea Kusini ikitoa tahadhari kwa Uganda
Mtu akipuliza dawa katika hema la matibabu ya Ebola eneo la Bunia, DRC / AP

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Urusi Maria Zakharova amesema siku ya Alhamisi kuwa Urusi ina wasiwasi kuhusu mlipuko wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Uganda na kwamba iko tayari kutatua tatizo hilo.

Maambukizi 51 ya Ebola yamethibitishwa Congo kufikia sasa, kulingana na Shirika la Afya Duniani.

Wakati huohuo siku ya Alhamisi Korea Kusini iliongeza kiwango chake cha tahadhari kuhusu kusafiri kwenda Uganda, Shirika la Habari la Yonhap liliripoti, baada ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki kubaini maambukizi mawili katika mji mkuu, Kampala, ikiwemo kifo cha mtu mmoja aliyesafiri kutoka Congo..

Wizara ya mambo ya nje ya Korea Kusini imeongeza hali ya tahadhari ya kusafiri Uganda kutoka Ngazi ya 2, ambayo inashauri kuhusu safari zisizo na ulazima, hadi kwa ushauri wa marufuku ya kutosafiri.

Futa safari

Serikali imetoa wito kwa raia wa Korea Kusini kufuta au kuahirisha safari za kwenda Uganda na kuwashauri wale walio katika nchi hiyo kuzingatia usalama wao.

Wizara hiyo pia inapanga kuagiza marufuku ya kusafiri ya Ngazi ya 4 kwa Mkoa wa Ituri katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Shirika la Kudhibiti Magonjwa la Korea siku ya Jumanne liliorodhesha Congo, Uganda na Sudan Kusini kama mataifa ambayo yanahitaji watu wanaotoka huko kuwekwa katika uangalizi kutokana na virusi vya Ebola.

Mlipuko huu wa sasa ni wa aina wa Bundibugyo, moja ya virusi ambavyo vinaweza kusababisha ugonjwa wa Ebola, kulingana na WHO.

CHANZO:TRT Afrika and agencies