Wizara ya Ulinzi ya Uturuki yasisitiza kuhusu umuhimu wa uthabiti wa mifumo ya anga ya nchi

Udhibiti wa anga ya Uturuki unahakikishwa saa 24/7, wizara hiyo inasema baada ya ndege isiyokuwa na rubani kudunguliwa katika Bahari Nyeusi.

By
Picha inaonesha mfumo wa ulinzi wa anga ya masafa marefu wa Uturuki Siper baada ya uzinduzi wa majaribio huko Sinop / AA / AA

Wizara ya Ulinzi ya Uturuki imesisitiza kuhusu uthabiti wa mifumo yake ya anga baada ya ndege isiyokuwa na rubani kudunguliwa katika Bahari Nyeusi.

"UAV hiyo ilifanyiwa tathmini na kuvunjwa vipande vipande na kuenezwa katika eneo hilo. Hii inafanya kuwa ngumu kutambua vipande hivyo vikiwa chini,” wizara ilisema siku ya Alhamisi.

Kulingana na wizara hiyo udhibiti wa anga ya Uturuki “umehakikishwa saa 24/7 katika ngazi mbalimbali ikiwemo mfumo wa rada, kuonya, vita vya teknolojia, na mifumo ya kuzuia.”

Wizara pia iliongeza kuwa imeonya pande zote mbili katika vita vinavyoendelea kati ya Ukraine na Urusi kuwa makini zaidi ili kuepusha matukio ambayo yanaweza kutatiza usalama katika Bahari Nyeusi.

Ndege isiyokuwa na rubani iligundulika kuwa nje ya udhibiti wakati ikikaribia anga ya Uturuki katika Bahari Nyeusi na kudunguliwa, Wizara ya Ulinzi ya Uturuki ilisema siku ya Jumatatu.

Kifaa kimoja kilikuwa katika anga ya Uturuki juu ya Bahari Nyeusi kiligunduliwa na kufuatiliwa kulingana na taratibu zilizopo, wizara imesema katika taarifa kupitia mtandano wa kijamii wa Uturuki wa NSosyal.

Kuhakikisha usalama wa anga za nchi, ndege zilizoidhinishwa na NATO na kudhibitiwa na taifa za F-16 zilipelekwa kwa ajili ya kujibu mashambulizi hayo, taarifa ilisema.

Kufuatia tathmini hiyo kifaa hicho cha angani kilijulikana kuwa ni ndege isiyo na rubani ambayo ilipoteza muelekeo, "ilidunguliwa katika sehemu salama mbali na maeneo yanayoishi watu ili kuepuka madhara yoyote," wizara iliongeza.