Shirika la Ndege la Uturuki kujenga kituo kikubwa zaidi cha mizigo kwa zaidi ya bilioni $2.3

Shirika la Ndege la Taifa la Uturuki pia litajenga sehemu ya huduma ya chakula kubwa zaidi duniani ya ndani ya ndege.

By
Mwisho wa 2025, Shirika la Ndege la Turkish Airlines ilikuwa na idadi ya ndege 514. / / AA

Shirika la Ndege la taifa la Uturuki, (Turkish Airlines), lilitangaza Ijumaa kuwa litajenga kituo kikubwa zaidi cha mizigo duniani pamoja na sehemu kubwa zaidi ya huduma za chakula ya ndani ya ndege, kwa uwekezaji wa lira za Uturuki bilioni 100 (zaidi ya dola bilioni 2.3 za Marekani).

“Uturuki inakua, “Turkish Airlines” inapaa juu,” shirika hilo liliandika kwenye jukwaa la mitandao ya kijamii la Kituruki, NSosyal.

Shirika hilo limesema kuwa uwekezaji huo na uanzishwaji wa kituo cha mizigo pamoja na sehemu ya upishi wa ndani ya ndege vitazalisha ajira mpya 26,000.

“Kama chapa ya bendera ya taifa ya Uturuki, fahari hii inatufanya tujivunie zaidi,” shirika hilo liliongeza.

Eneo la miradi hiyo halikutajwa, lakini Istanbul—mji mkuu wa kibiashara wa Uturuki na mwenye vituo viwili vikubwa vya kimataifa vya usafiri wa anga—una uwezekano mkubwa kuwa mahali pa miradi hiyo.

Turkish Airlines yenye makao yake Istanbul ni miongoni mwa mashirika makubwa zaidi ya ndege duniani, ikisafirisha zaidi ya abiria milioni 85 na tani milioni 2 za mizigo kwa mwaka.

Jumanne, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Bilal Eksi, alisema kuwa kufikia mwaka 2033 watakuwa miongoni mwa mashirika matano bora zaidi ya ndege duniani, wakati watakapofikia idadi ya ndege 813.

Mwisho wa mwaka 2025, Turkish Airlines ilikuwa na ndege 514.