| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Sudan yaahidi kukabiliana na mfumuko wa bei huku vita vikiathiri uchumi
Sudan imeahidi kushusha mfumuko wa bei hadi chini ya 60% kufikia mwisho wa mwaka 2026, huku miaka mitatu ya vita ikiacha raia wakikabiliwa na tatizo na gharama za maisha.
Sudan yaahidi kukabiliana na mfumuko wa bei huku vita vikiathiri uchumi
Sudan imekabiliwa na mfumuko wa bei tangu kuanza kwa vita Aprili 2023.

Sudan imeahidi kushusha mfumuko wa bei hadi chini ya 60% kufikia mwisho wa mwaka 2026, huku miaka mitatu ya vita ikiacha raia wakikabiliwa na tatizo na gharama za maisha.

Nchi hiyo imekabiliana na mfumuko mbaya wa bei kwa miaka kadhaa, lakini tangu vita kuanza kati ya jeshi na wapiganaji wa Rapid Support Forces (RSF) tangu Aprili 2023, uchumi ambayo ulikuwa ukisuwasuwa nchini humo umezorota zaidi.

Na vita vya Marekani na Iran pia vimesababisha bei ya nishati kupanda kote duniani, Sudan ina jukumu kubwa la kukabiliana na kupanda kwa gharama za bidhaa.

Akizungumza katika Mkutano wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) siku ya Jumatatu, Waziri wa Fedha Gibril Ibrahim anasema "tunatarajia kupunguza mfumuko wa bei hadi chini ya asilimia 60 kufikia mwisho wa mwaka 2026."

Uchumi umezorota

"Viashiria hivyo vinaonesha kuwa inawezekana," aliongeza. Mfumuko wa bei kwa sasa ni 99% mwaka 2025, kufuatia kufikia hadi 176% mwaka 2024, kulingana na Ibrahim, ambaye kauli yake ilitangazwa kupitia televisheni ya taifa.

Mwezi huu, ubadilishaji wa dola moja ya Marekani ulikuwa sawa na zaidi ya pauni 8,000 za Sudan, mara 16 kabla ya vita.

"Bei zinabadilika kila siku kulingana na thamani ya dola," alisema muuza duka wa mjini Khartoum Ibrahim Mohammad Ahmed. "Watu wanalazimika kuacha mambo mengine muhimu," aliongeza.

Vita hivyo vimesababisha vifo vya maelfu ya watu, na kuwaacha mamilioni wengine bila makazi, na kuharibu vibaya uchumi wa nchi.

Ripoti ya Kamati ya Walimu wa Sudan inasema kuwa kwa sasa familia moja inahitaji karibu $600 kwa mwezi kwa mahitaji yake. Cha kushangaza, walimu wanapata mshahara wa karibu $19 kwa mwezi.

CHANZO:Anadolu Agency