Marie-Louise Eta: Mwanamama aliyepewa mikoba Bundesliga
Marie-Louise Eta amepewa jukumu la kuiongoza klabu ya Union Berlin kwa miezi miwili, mpaka Juni mwaka huu./Picha:Reuters
Marie-Louise Eta: Mwanamama aliyepewa mikoba Bundesliga
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 34, anaingia kwenye vitabu vya historia, kwa kuwa mwanamke wa kwanza katika ligi kuu tano bora barani Ulaya, kufundisha timu ya soka ya wanaume.

Huko nchini Ujerumani, stori kubwa kwa sasa ni Marie-Louise Eta.

Mwanamama huyu ameteuliwa kuifundisha timu ya soka ya wanaume ya Union Berlin inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani, maarufu kama Bundesliga.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 34, anaingia kwenye vitabu vya historia, kwa kuwa mwanamke wa kwanza katika ligi kuu tano bora barani Ulaya, kufundisha timu ya soka ya wanaume.

Marie-Louise Eta amepewa jukumu la kuiongoza klabu ya Union Berlin kwa miezi miwili, mpaka Juni mwaka huu.

Uamuzi wa kumpa mikoba mwanamama huyu jukumu hilo kubwa, linafuatia mechi ya hivi karibuni, ambapo Union Berlin ilipoteza kwa mabao 3-1 dhidi ya Heidenheim, na klabu hiyo kulazimika kumtimua aliyekuwa kocha wake, Steffen Baumgart.

Kibarua kinachomsubiri Marie-Louise Eta kwa sasa, ni kuinasua Union Berlin kutoka nafasi yake ya 11 kwenye msimamo wa Bundesliga.

Hata hivyo, hilo si jambo geni kwa bara la Afrika.

Mwaka 2024, Jackline Juma alikuwa mwanamke wa kwanza kufundisha timu ya soka ya wanaume, baada ya kuiongoza klabu ya Talanta, iliyokuwa ikishiriki ligi kuu ya KPL nchini Kenya.

Mwaka huo huo, Oliver Mbekeka alipewa jukumu la kuifundisha klabu ya Lugazi iliyokuwa ikishiriki ligi kuu ya nchini Uganda, na kuwa mwanamke wa kwanza nchini humo kufundisha timu ya wanaume.

Oliver alichukua mikoba hiyo kufuatia kuondoka kwa kocha Sadiq Ssempigi na atakumbukwa kwa kuiongoza Lugazi kuifunga klabu ya Express kwa bao 1-0 kwenye uwanja wa Nakivubo.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Soma zaidi
Wanigeria wanajiunga na Wakenya, Waghana kama wafanyakazi wanaotafutwa sana na makampuni ya Marekani
Zaidi ya fidia: Mustakbali wa Afrika unahitaji mtazamo mpya sio malipo
Polisi Afrika Kusini wawakamata watu zaidi 1,000 katika msako wa wahalifu
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Congo Makosso ajiuzulu
Watu kumi na nne waliotekwa Nigeria waokolewa: Gavana wa Jimbo
Ziara ya Afrika: Papa Leo afanya Misa nchini Angola
Wamefukuzwa Sahel: Ufaransa inatafuta nini nchini Kenya?
Pande zinazopigana DR Congo zimekubaliana kubadilishana wafungwa na kuruhusu ufikiaji wa msaada
Nigeria yavamia ‘kiwanda cha watoto’ huko Lagos, na kuwaokoa wanawake wajawazito
Marekani yawawekea vikwazo wapiganaji wa Colombia nchini Sudan
Kundi la kwanza la waliofukuzwa kutoka Marekani lawasili Kinshasa nchini DRC
Mtoto wa Mugabe akiri kumtishia mtu kwa bunduki nchini Afrika Kusini
Nigeria yapiga marufuku kusimikwa kwa ‘Wafalme wa Igbo’ nje ya nchi
Mawaziri wa mambo ya nje wa Uturuki, Misri, Pakistan, Saudia kukutana Jukwaa la Diplomasia Antalya
Somalia inasema hatua ya Israel kuunga mkono Somaliland inakiuka Uhuru wa Somalia
Mwakilishi Maalumu wa Jumuiya ya Madola Lazarus Chakwera ahitimisha ziara yake nchini Tanzania
Kenya yaomba msaada wa haraka kutoka Benki ya Dunia huku ikipunguza VAT
Wadau wajadili fursa za uwekezaji katika Kongamano la Biashara linaloendelea Kigoma, Tanzania
Mbunge Tanzania ataka sekta binafsi iruhusiwe uzalishaji wa nishati ya umeme
Kampuni ya BP yashtakiwa Kenya kufuatia madai ya uchafuzi mazingira kutokana na uchimbaji mafuta