Iran yarusha makombora ya balistiki Israel, yaua 9 Beit Shemesh, 12 nchi nzima
Shambulizi baya zaidi limefanyika Jumapili, Beit Shemesh, mji wa magharibi mwa Jerusalem, ambapo kombora la balistiki la Iran lilipiga moja kwa moja eneo la jirani.
Iran imeongeza kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasa kwa kutumia makombora ya 'balistic' dhidi ya Israel kufuatia mashambulizi ya pamoja ya Marekani na Israel ambayo yamesababisha kifo cha kiongozi wa dini Ali Khamenei.
Waliouawa kwa upande wa Israel kutokana na mashambulizi ya Iran wamefikia takriban 12 na zaidi ya 150 kujeruhiwa, kwa mujibu wa vyanzo kutoka Israel.
Mifumo wa ulinzi ya Israel, ikiwemo Iron Dome, David's Sling, na Arrow, imedungua sehemu kubwa ya makombora, lakini baadhi yamekuwa na athari za moja kwa moja kwa raia.
Shambulizi baya zaidi limefanyika Jumapili, Beit Shemesh, mji wa magharibi mwa Jerusalem, ambapo kombora la balistiki la Iran lilipiga moja kwa moja eneo la jirani.
Kombora liliharibu majengo kadhaa, ikiwemo eneo la kujikinga na mabomu, na kusababisha kuanguka kwa sehemu ya juu.
Magen David Adom (MDA), kitengo cha taifa cha dharura cha huduma ya afya, awali kiliripoti kuongezeka kwa vifo kutwa nzima, kutoka watu sita hadi wanane, baadaye kufikia watu tisa, huku wengi zaidi wakijeruhiwa, wawili wakiwa katika hali mbaya zaidi.
Gazeti la Times of Israel limeripoti idadi ya vifo katika eneo la Beit Shemesh imefikia tisa, huku likielezea uharibifu mkubwa katika makazi ya watu na maeneo ya kujikinga.