Unatumia Gaza kwa majaribio ya silaha: Waandamanaji wakabili maonyesho ya silaha huko Tel Aviv

Waandamanaji wanashutumu mashirika ya ulinzi ya Israeli kwa kufaidika kutokana na vita huku makampuni kadhaa yakionyesha silaha "zilizothibitishwa".

By
Wanaharakati wafanya maandamano katika maonyesho ya teknolojia ya silaha mjini Tel Aviv. / AA / AA

Waandamanaji wa Israel wamekusanyika nje ya maonesho makubwa ya silaha mjini Tel Aviv, na kuyatuhumu makampuni yanayotengeza silaha kwa kutumia Gaza kama "eneo la majaribio" ya silaha.

Maandamano yamefanyika nje ya Maonesho ya Silaha ya mwaka 2026 siku ya Jumanne, maonesho ya kimataifa ya silaha yanayofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Maonesho wa Tel Aviv.

Takriban waandamanaji 20 walibeba mabango yanayosoma, "Mnatumia Gaza kama sehemu ya majaribio" na kuitisha vikwazo vya silaha, na kupinga kile walichokieleza kama njia ya kujipatia faida katika mauaji ya halaiki yanayofanywa na Israel huko Gaza.

Maandamano hayo yaliratibiwa na kundi la Israeli ambalo halikutaka kutajwa kwa sababu za usalama.

Katika taarifa yake, kundi hilo limesema linaungana dhidi ya "faida inayotokana na sekta ya ulinzi dhidi ya ubaguzi na mauaji ya halaiki Gaza" na kulaani makampuni yanayoshiriki maonesho na wanunuaji wa kigeni waliohudhuria.

Kwa mujibu wa mtandao rasmi wa maonesho hayo, zaidi ya makampuni 70 ya Israel yaliyobobea katika ulinzi na silaha yanaonesha teknolojia za hali ya juu ambazo zinaelezwa "kufanyiwa majaribio."

Gazeti la kila siku la Israel Yedioth Ahronoth limeripoti mwanzoni mwa mwezi huu kwamba, onesho hilo, lililoratibiwa na Star Group, linatarajiwa kuvutia wageni kadhaa kutoka nje, ikiwemo maafisa waandamizi na wawekezaji katika teknolojia.

Onesho hilo pia limeandaliwa chini ya usimamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel, Wizara ya Biashara, Taasisi ya Uuzaji nje ya Israel na Muungano wa Wafanyabiashara wa Israel.

Maandamano hayo pia yanafanyika huku kukiwa na shinikizo la kuangaliwa kwa kina kwa aina ya silaha zinazotumiwa na Israel huko Gaza.

Mwezi FebruarI, ripoti ya uchunguzi iliyorushwa na Al Jazeera ilisema kuwa vikosi vya Israel vimetumia silaha zenye uharibifu mkubwa katika vita hivyo, ushuhuda uliotolewa na madaktari na maafisa wa usalama.

Makubaliano ya usitishaji wa mapigano yaliyosimamiwa na Marekani yalianza Oktoba 19, ambayo kwa kiasi fulani yamepunguza mauaji ya halaiki Gaza ambayo yameua zaidi ya watu 72,000, wengi wao wanawake na watoto, na kujeruhi zaidi ya 171,000 tangu Oktoba 2023.

Tangu kufanyika kwa makubaliano hayo Oktoba 10, vikosi vya Israel vimekiuka mara kadhaa kwa kufanya mashambulizi, na kuuwa Wapalestina 603 na kujeruhi 1,618, ka mujibu wa Wizara ya Afya ya Gaza.