Utajiri wa Afrika: Morocco, asili yamafuta ya argan

Mafuta ya argan hutengenezwa kutoka mbegu za matunda ya miti ya argan hii na hutumiwa katika kupikia na vipodozi ikiwa na sifa ya kulainisha ngozi na nywele.

By Coletta Wanjohi
The Argan tree in Morocco / Reuters

Utajiri wa Afrika: Mti wa argan wa Morocco

Morocco inaongoza kimataifa kwa uzalishaji wa moja ya miti mikongwe inayoitwa argan.

Mti wa argan ni spishi ya kawaida ya misitu inayoaminika kuwepo kwa zaidi ya miaka milioni 80 iliyopita kusini mwa Morocco.

Miti hii hukua tu katika maeneo kame ya Kusini-Magharibi mwa nchi, ambayo imeenea kwa zaidi ya hekta 800,000.

Mti ya Argan una uwezo mkubwa wa kustahimili mabadiliko ya hali ya hewa.

Ni maarufu kwa kuzalisha mafuta ya argan, ambayo ni zao kuu la mti wa argan na labda bidhaa yake inayojulikana zaidi duniani kote.

Mafuta ya argan hutengenezwa kutoka mbegu za matunda ya miti hii na hutumiwa katika kupikia na vipodozi ikiwa na sifa ya kulainisha ngozi na nywele.

Utengezaji wa mafuta kutoka matunda ya argan ni mchakato mrefu, na unafanywa hasa na wanawake.

Baada ya uvunaji wa matunda, hukaushwa na kusagwa, na hatimae kuchanganywa.

Kinu maalum cha mkono kinachotengenezwa na mafundi wa ndani hutumka kupiga piga na kuchanganya kunahusisha kuongeza taratibu kwa maji ya joto kwa kiasi halisi.

Kwa kweli, kilo 50 za matunda zinahitajika ili kuzalisha nusu lita tu ya mafuta, na ndiyo sababu bei ya soko la mafuta ya argan kawaida iko juu zaidi kuliko mafuta aina nyengine.

Tangu miaka ya 1990 wakati thamani ya vipodozi na matibabu ya mafuta ya argan ilipojulikana zaidi, bidhaa hiyo kidogo imekuwa adimu katika soko la kimataifa.

Mafuta ya argan, kwa karne nyingi yametumika na watu wa Berber wa Morocco kutibu magonjwa ya ngozi, maumivu ya misuli na ugonjwa wa moyo.

Mti wa argan unaweza kustahimili halijoto hadi 50°C na husaidia kupunguza kasi ya kuenea kwa jangwa. Unachangia maisha na usalama wa chakula katika jamii za kikanda.

Unga wa mbegu ambao mafuta hutolewa hutumika kama chakula cha mifugo kwa kondoo, mbuzi, ngamia, na ng'ombe.

Mafuta ya argan hutolewa kama zawadi ya harusi na hutumiwa sana katika utayarishaji wa sahani katika sherehe.

Ujuzi wa maandalizi ya mafuta na matumizi yake hupitishwa kwa 'wanawake wa argan', ambao huwafundisha binti zao wakiwa na umri mdogo.

Miti hii yenye uwezo wa kuishi kwa miaka 200 ilitambuliwa na UNESCO kama urithi muhimu 2014.

Vipengele vyote vya kitamaduni vya mti wa argan zinachangia uwiano wa kijamii, kuelewana kati ya watu binafsi na kuheshimiana kati ya jamii nchini Morocco.