Eritrea yataka Baraza la Usalama la UN itoe tamko juu ya kutambuliwa kwa Somaliland na Israel
Eritrea imetaka kutolewa kwa tamko kutoka kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya kutambuliwa kwa Somaliland na Israel, ikionya kwamba hatua hiyo inaweza kuchochea ukosefu wa usalama kikanda na kimataifa.
Eritrea inalitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutoa tamko 'lenye uthubutu' juu ya uamuzi wa Israel wa kutambua Somaliland, ikionya kwamba hatua hiyo inaweza kuchochea ukosefu wa usalama kikanda na kimataifa.
Wizara ya Habari ilisema katika taarifa Jumapili kwamba 'njama' hiyo si 'siri ambayo ilikuwa haifahamiki' bali imekuwa 'ikiandaliwa' kwa muda, na inaweza kusababisha 'migogoro hatari ya kikanda na kimataifa, pamoja na vurugu'.
'Kwa hivyo, inastahili tamko lenye uthubutu katika ngazi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na wanachama wake,' iliongeza taarifa.
Ijumaa, Israel ilitangaza kutambua Somaliland, jambo lililosababisha kushtumiwa na taifa la Somalia, nchi zingine kadhaa pamoja na Umoja wa Afrika.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litajadili suala hilo Jumatatu.
Somaliland ilitengana na Somalia mwaka 1991, hatua ambayo haitambuliwi na Somalia wala jamii ya kimataifa.
Eritrea na Somalia zilirudisha uhusiano wa kidiplomasia mwaka 2018 baada ya miaka kadhaa ya taharuki, na tangu wakati huo zimeimarisha ushirikiano katika masuala ya usalama katika kanda.
Baraza la Usalama linatarajiwa kujadili suala la Israel kutambuwa Somaliland katika kikao cha dharura siku ya Jumatatu.