Uganda yazuia raia wa Marekani na Umoja wa Ulaya kuingia bila viza
Uganda imetoa orodha ya raia kutoka mataifa 40 ambao wanaruhusiwa kuingia bila viza, ambapo raia wa Marekani na Umoja wa Ulaya hawapo katika orodha hiyo.
Uganda imetangaza kuingia bila viza kwa raia kutoka mataifa 40, ikiondoa Marekani na nchi za Umoja wa Ulaya katika orodha hiyo.
Huu ni mpangilio mpya.
Kulingana na serikali ya Uganda, wasafiri kutoka nchi zilizoorodheshwa hawatahitajika tena kupata viza kabla ya kusafiri hadi Uganda na wanaweza kukaa hadi miezi mitatu kwa utalii au biashara.
Nchi za Afrika ambazo hazitakiwi kupata viza kabla ya kusafiri kwenda Uganda ni Kenya, Tanzania, Rwanda, Uganda, Burundi, Sudan Kusini, Seychelles, Mauritius, Msumbiji, Zambia, Zimbabwe, Malawi, Botswana, Lesotho, Madagascar, Comoro, Eritrea, Gambia, Sierra Leone, Ghana na Eswatini.
Wengine watalazimika kutafuta viza na kungoja kuidhinishwa kuingia katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
"Uamuzi huu mpya unarahisisha usafiri na kuakisi kujitolea kuendelea kwa Uganda katika kukuza ushirikiano wa kikanda, utalii, biashara, na muunganisho kati ya watu na watu," imesema Serikali ya Uganda kupitia ukurasa wake wa X.
Nchi za Marekani na Umoja wa Ulaya zimetengwa
Nchi nyingine zisizo za Kiafrika ambazo zina fursa ya kuingia Uganda bila viza ni:
Ireland, Jamaica, Antigua na Barbuda, Bahamas, Barbados, Belize, Cyprus, Fiji, Grenada, Malaysia, Malta, Singapore, Visiwa vya Solomon, St. Vincent na Grenadines, Tonga, Trinidad na Tobago, Falme za Kiarabu, Vanuatu na Hong Kong SAR.
Marekani na nchi kutoka Umoja wa Ulaya pamoja na Uingereza hazijapata fursa ya kuingia nchini Uganda bila viza.
Mabadiliko ya sera ya viza na kuingia nchini Uganda yanafuatia uamuzi wa Marekani wa kuanzia Januari 21, 2026, ulioweka sheria kali za viza kwa Uganda.
Hii ni pamoja na dhamana inayoweza kurejeshwa ya $15,000 kwa visa vya B1/B2, uhalali uliopunguzwa hadi miezi 3 na vizuizi vya kuingia mara moja.
Uganda pia imepunguza idadi ya nchi ambazo zina fursa ya kupata hati ya kusafiria za kidiplomasia.
"Sera hii inaunga mkono ziara rasmi, mashirikiano ya hali ya juu, na ushirikiano mkubwa kati ya nchi mbili," imefafanua.
Nchi zinazoshughulikiwa kwa sasa ni Algeria, Cuba, Misri, Ethiopia, India, Iran, Urusi, Senegal, Afrika Kusini, Uturuki ( kwa wanadiplomasia tu) Venezuela, na Vietnam.