UTURUKI
3 dk kusoma
Ziara ya Erdogan Ghuba: Uturuki, Qatar zasaini mikataba ya ulinzi na ushirikiano wa kimkakati
Erdogan na Al Thani wameshuhudia utiaji saini wa mikataba kadhaa kati ya nchi zao baada ya kuongoza kwa pamoja Mkutano wa 11 wa Kamati ya Juu ya Ushirikiano wa Kimkakati jijini Doha, Qatar.
Ziara ya Erdogan Ghuba: Uturuki, Qatar zasaini mikataba ya ulinzi na ushirikiano wa kimkakati
Qatar ni kituo cha pili cha ziara ya siku tatu ya Ghuba ya Erdogan, ambayo pia inajumuisha nchi ya Oman. / / AA
tokea masaa 8

Uturuki na Qatar zimetia saini makubaliano kadhaa na azimio la pamoja kama sehemu ya Mkutano wa 11 wa Kamati ya Juu ya Ushirikiano wa Kimkakati kati ya Uturuki na Qatar.

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, na Emir wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, wameshuhudia utiaji saini wa mikataba mbalimbali kati ya nchi zao baada ya kuongoza kwa pamoja Mkutano wa 11 wa Kamati ya Juu ya Ushirikiano wa Kimkakati uliofanyika jijini Doha, Qatar.

Awali, viongozi hao walikutana faraghani na pia wakafanya mazungumzo kati ya wajumbe wa pande zote katika kasri ya Emir wa Qatar.

Mikataba iliyotiwa saini ni pamoja na:

“Azimio la Pamoja la Mkutano wa 11 wa Kamati ya Juu ya Ushirikiano wa Kimkakati kati ya Jamhuri ya Uturuki na Nchi ya Qatar”, lilitiwa saini na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan, na Waziri Mkuu wa Qatar ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani.

"Mkataba wa Maelewano kati ya Kiongozi wa Mkakati na Bajeti ya Jamhuri ya Uturuki na Nchi ya Qatar juu ya Ushirikiano na Kubadilishana Uzoefu katika Nyanja Mbalimbali ya Mipango ya Maendeleo ya Kimkakati" ulitiwa saini na Waziri wa Hazina na Fedha wa Uturuki Mehmet Simsek, Waziri wa Biashara Omer Bolat, na Katibu Mkuu wa Baraza la Mipango la Kitaifa la Qatar Nalifaz Allifaz Alfabin Khalifa.

“Azimio la Pamoja la Mawaziri kati ya Wizara ya Biashara ya Uturuki na Wizara ya Biashara na Viwanda ya Qatar, lilitiwa saini na Waziri wa Biashara wa Uturuki, Omer Bolat, na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Qatar, Sheikh Faisal bin Thani Al Thani.

“Makubaliano ya Ushirikiano katika Sekta ya Ulinzi na Viwanda vya Kijeshi”, yalisainiwa na Rais wa Shirika la Viwanda vya Ulinzi la Uturuki, Haluk Gorgun, na Naibu Waziri Mkuu wa Qatar ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi, Sheikh Saud bin Abdulrahman bin Hassan bin Ali Al Thani.

Utulivu wa dunia

Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki, mkutano huo pia uliangazia mahusiano ya mataifa mawili pamoja na masuala ya kikanda na kimataifa.

"Rais Erdogan alisema kuwa Uturuki inalenga kuimarisha zaidi uhusiano wake bora na Qatar, ambayo kwa sasa unaonyesha mafinikio makubwa katika nyanja mbalimbali kama vile ushirikiano wa kijeshi, sekta ya ulinzi, nishati, biashara na uwekezaji," aliongeza.

Aidha, Erdogana alieleza kuwa ushirikiano wa kimkakati kati ya Uturuki na Qatar unachangia kwa kiasi kikubwa katika utulivu wa kikanda na duniani kwa ujumla.

Kuhusu Gaza, Erdogan alisema kwamba makubaliano ya hivi karibuni ya kusitisha mapigano yameleta afueni inayohitajika kwa Wapalestina, na akasisitiza kuwa suluhisho la mataifa mawili ndilo suluhisho pekee linaloweza kufanyiwa kazi katika mzozo kati ya Israel na Palestina, na juhudi kuelekea suluhisho hilo zitaendelea.

"Rais Erdogan alisema kuwa Uturuki itaunga mkono mchakato wa kujenga upya Syria na kwamba ushirikiano na Qatar utaendelea katika nyanja zote husika nchini Syria, ikiwa ni pamoja na nishati, usafiri, na misaada ya kibinadamu," kurugenzi hiyo ilisema.

Baada ya ziara yake rasmi nchini Qatar, Rais Erdogan na ujumbe wake walielekea nchini Oman siku ya Jumatano, ambayo ni kituo cha mwisho katika ziara yake ya siku tatu katika nchi za Ghuba.

CHANZO:TRT World