Morocco yatangaza kumalizika kwa miaka saba ya kiangazi baada ya mvua za msimu wa baridi
Kiangazi cha miaka saba nchini Morocco kimemamilizika baada ya mvua za msimu wa baridi, Waziri wa Maji Nizar Baraka alisema siku ya Jumatatu.
Miaka saba ya kiangazi nchini Morocco imefikia kikomo baada ya mvua za msimu wa baridi kali, Waziri wa Maji Nizar Baraka amesema siku ya Jumatatu.
Mvua za msimu huu wa baridi ni 95% zaidi ikilinganishwa na kipindi kama hiki mwaka mmoja uliopita na 17% zaidi ya wastani kwa msimu, Baraka amewaambia wabunge.
Kujaza mabwawa kumeongezeka kwa 46%, huku hifadhi za maji zikijaa pomoni, takwimu rasmi zinaonesha.
Mvua hizo zimeleta afuweni kubwa kwa sekta ya kilimo baada ya miaka kadhaa ya uhabad wa maji.
Athari za kiangazi
Miaka saba ya kiangazi yamemaliza maji katika mabwawa ya Morocco, kupunguza mavuno ya ngano, kupungua kwa idadi ya mifugo, kusababisba watu kupoteza ajira katika sekta ya kilimo.
Morocco inalenga kusambaza 60% ya maji ya kunywa kutokana na maji ya bahari yaliyotia dawa kufikia 2030, kutoka 25%, na kuacha maji ya mabwawa mwa ajili ya maeneo ya mbali ya nchi, Baraka aliiambia Reuters Disemba.