| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Uturuki kuwa mwenyeji wa mkutano wa mazingira wa COP31 baada ya makubaliano na Australia
Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese anasema Waziri wa Mabadiliko ya Tabianchi Chris Bowen atakuwa Rais wa COP katika mashauriano, huku Uturuki ikiwa mwenyeji wa mkutano na Urais wa COP.
Uturuki kuwa mwenyeji wa mkutano wa mazingira wa COP31 baada ya makubaliano na Australia
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akizungumza wakati wa Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi wa COP29 UN, Novemba 12, 2024, Baku, Azerbaijan. / TRT Afrika Swahili
20 Novemba 2025

Uturuki itakuwa mwenyeji wa mkutano wa mwakani wa COP31 wa mabadiliko ya tabianchi katika mji wa Mediterani wa Antalya baada ya Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese kutangaza kuwa nchi yake imejiondoa.

"Kilichoafikiwa ni kwamba (Waziri wa Mabadiliko ya Tabianchi) Chris Bowen, Australia, atakuwa Rais wa COP wa mashauriano.

"Kongamano na Urais wa COP utakuwa wa Uturuki, na kutakuwa na mkutano wa kabla ya COP, hasa kuangazia ufadhili wa mabadiliko ya hali ya hewa katika eneo la Pasifiki, kupitia ‘‘the Pacific Resilience Facility’’, katika maandalizi ya mkutano wa COP mwakani, utakaofanyika eneo la Pasifiki," Albanese aliliambia shirika la habari za umma la Australia ABC Radio Perth.

Aliyaelezea makubaliano hayo kama "ushindi mkubwa kwa wote Australia na Uturuki".

"Sheria za mikutano ya tabianchi ni kwamba inatakiwa ifanyike kwa makubaliano," alisema. "Kama siyo makubaliano, pengine mji wa Bonn, Ujerumani ndiyo ungekuwa mwenyeji."

CHANZO:AA