| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Somalia yaanza usajili wa meli kwa kutumia bendera yake ya taifa
Hatua hiyo inafuatia serikali ya Somalia kupitisha sheria za ndani na kanuni ya kimataifa yenye kuruhusu usajili wa meli kwa kutumia bendera ya Somalia.
Somalia yaanza usajili wa meli kwa kutumia bendera yake ya taifa
Usajili wa meli kwa kutumia bendera ya Somalia./Picha:Wengine
tokea masaa 3

Somalia imefanikiwa kusajili chombo kimoja cha baharini kwa kutumia bendera ya taifa ya nchi hiyo, miaka 35 tangu kuibuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo, mwaka 1991.

Kulingana na Waziri wa Bandari na Uchukuzi wa Somalia, Abdulkadir Mohamed Nur, hatua hiyo inaashiria mwanzo mpya wa sekta ya majini ya Somalia.

 “Leo hii tumefanikiwa kusajili chombo kiitwacho 'Guney' kwa kutumia bendera ya Somalia,” alisema waziri huyo.

Nur alitumia nafasi hiyo kuwavuta wafanyabiashara na wamiliki wengine wa meli kutumia fursa ya kusajili vyombo vyao kwa kutumia bendera ya Somalia.

Hatua hiyo inafuatia serikali ya Somalia kupitisha sheria za ndani na kanuni ya kimataifa yenye kuruhusu usajili wa meli kwa kutumia bendera ya Somalia.