Turkish Airlines yaongeza idadi ya ndege

Shirika hilo limeongeza idadi ya ndege zake kutoka 65 mwaka 2003 hadi kufikia 531, mwaka huu.

By
Shirika la ndege la Uturuki./Picha:Reuters

Shirika la ndege la Uturuki limeongoza idadi ya ndege na kufikia 531, ndani ya miongo miwili.

"Hatujaacha, bado tunaendelea kukua,” alisema Afisa Mtendaji wa Turkish Airlines Bilal Eksi.

"Kufikia mwaka 2003, ndege zetu zilikuwa 65, leo hii tunajisikia kufikia idadi ya 531,” aliongeza.

Disemba 2024, shirika la ndege Uturuki lilipata hadhi ya rekodi za dunia za Guinness, kwa kuwa lenye kufika nchi nyingi zaidi.

Shirika hilo ni moja kati ya mashirika makubwa duniani, likisafirisha abiria milioni 85 na tani milioni 2 za mizigo kwa mwaka.