Droni zilizorushwa na Ukraine zimeua watu wanne, akiwemo mtoto mmoja katika eneo la makazi katika mji wa Ryazan, kusini magharibi mwa Moscow.
Tukio hilo linafuatia shambulio la awali lililofanywa na Urusi dhidi ya Ukraine, na kuua watu 24 huko Kiev.
"Usiku wa leo, eneo la Ryazan lilishambuliwa na droni zipatazo 99 kutoka kwa maadui zetu,” alisema," gavana wa Ryazan, Pavel Malkov.
“Kwa bahati mbaya, idadi ya vifo imeongezeka na kufikia wanne, akiwemo mtoto mdogo, huku wengine saba wakipokea matibabu."
Tathmini ya tukio hilo, bado inaendelea kulingana na Malkov.
Kwa upande wake, timu ya uchunguzi ya Urusi, ilisema ilikuwa inalichunguza tukio hilo, ikisisitiza kuwa lilikuwa ni shambulizi dhidi ya miondombinu ya makazi na raia.
CHANZO:AFP












